Sagittarius A*

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya kwanza ya Sagitarius A* iliotolewa Mei, 2022.

Sagittarius A*, kwa ufupi Sgr A* ni shimo jeusi katika kiini cha galaksi ya Njia nyeupe,[1][2][3] lenye tungamo wa takriban milioni 4.3 wa Jua.[4][5] Iko karibu na mpaka wa makundinyota ya Mshale na Nge, karibu 5.6° kusini mwa njia ya Jua,[6] karibu na Fungu la Kipepeo (M6)[7] na Shaula (λ Scorpii)[8].

Kitu hicho ni chenye kung'aa sana, na chanzo cha redio za angani na chenye mchanganyiko mkubwa wa mahala pamoja. Jina Sagittarius A* linafuata kutokana na sababu za kihistoria. Mwaka 1954[9] John D. Kraus, Hsien-Ching Ko, na Sean Matt waliorodhesha vyanzo vya redio walivyovitambulika kwa darubini ya redio ya Chuo Kikuu cha Ohio State[10] katika 250 MHz (mawimbi ya redio). Vyanzo hivyo vilipangwa na kundi la nyota na barua waliyopewa ilikuwa haielewwki, huku A ikiashiria chanzo cha redio angavu zaidi ndani ya kundi hilo. Asterisk ni kwa sababu ugunduzi wake ulichukuliwa kuwa "wa kusisimua"[11], sambamba na nomenclature kwa atomi za hali ya kusisimua ambazo zinaonyeshwa na asterisk (kwa mfano hali ya kusisimua ya Helium ingekuwa He*). Asterisk ilipewa (andikwa na_) na Robert L. Brown, mwaka 1982[12], ambaye alielewa kuwa uzalishaji mkubwa wa mawimbi redio kutoka katikati ya galaksi ulionekana ni kutokana na compact nonthermal radio object (kitu chenye mgandamizo mkubwa ya mawimbi redio).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Jeff Parsons (2018-10-31). Scientists find proof a black hole is lurking at the centre of our galaxy (en). Metro. Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
 2. A 'mind-boggling' telescope observation has revealed the point of no return for our galaxy's monster black hole - The Middletown Press. web.archive.org (2018-10-31). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-10-31. Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
 3. Astronomers see material orbiting a black hole *right* at the edge of forever (en-US). SYFY Official Site (2018-11-07). Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
 4. Brooke Boen (2015-05-20). Supermassive Black Hole Sagittarius A*. NASA. Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
 5. Revnivtsev, M. G.; Churazov, E. M.; Sazonov, S. Yu; Sunyaev, R. A.; Lutovinov, A. A.; Gilfanov, M. R.; Vikhlinin, A. A.; Shtykovsky, P. E. et al. (2004-10-01). "Hard X-ray view of the past activity of Sgr A in a natural Compton mirror" (in en). Astronomy & Astrophysics 425 (3): L49–L52. doi:10.1051/0004-6361:200400064 . ISSN 0004-6361 . https://www.aanda.org/articles/aa/abs/2004/39/aagh113/aagh113.html.
 6. Scott MacNeill. Equatorial and Ecliptic Coordinates (en). Frosty Drew Observatory & Sky Theatre. Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
 7. "Butterfly Cluster", Wikipedia (in English), 2022-12-09, retrieved 2022-12-13 
 8. "Lambda Scorpii", Wikipedia (in English), 2022-11-28, retrieved 2022-12-13 
 9. Kraus, J. D.; Ko, H. C.; Matt, S. (1954-12-01). "Galactic and localized source observations at 250 megacycles per second.". The Astronomical Journal 59: 439–443. doi:10.1086/107059 . ISSN 0004-6256 . https://ui.adsabs.harvard.edu/abs/1954AJ.....59..439K.
 10. "Ohio State University", Wikipedia (in English), 2022-12-09, retrieved 2022-12-13 
 11. Goss, W. M.; Brown, Robert L.; Lo, K. Y. (2003-09). "The Discovery of Sgr A*" (in en). Astronomische Nachrichten 324 (S1): 497–504. doi:10.1002/asna.200385047 . ISSN 0004-6337 . https://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1002/asna.200385047.
 12. 1982ApJ...262..110B Page 110. adsabs.harvard.edu. Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sagittarius A* kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.