Russell Westbrook

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Russell Westbrook akiwa anachezea timu ya kikapu ya Oklohama City Thunder mwaka 2017
Westbrook akiwa na timu ya Los Angeles Lakers 2022

Russell Westbrook III[1] (alizaliwa 12 Novemba 1989) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea Marekani anayeichezea timu ya Los Angeles Clippers katika Chama cha mpira wa kikapu Marekani (NBA). Ni Mwanachama wa Timu ya Maadhimisho ya Miaka 75 ya Chama cha mpira wa kikapu Marekani (NBA 75th Anniversary Team), amefanikiwa kuteuliwa kama nyota wa mpira wa kikapu marekani (NBA All-Star) mara tisa na alipata tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi (MVP) katika msimu wa 2016-2017. Yeye pia ni mwanachama wa Timu ya Nyota wa NBA (All-NBA) mara tisa, katika misimu miwili ya 2014-2015 na 2016-17 aliongoza kama mchezaji mwenye magoli mengi na pia alishinda mfululizo mara mbili tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi katka mchezo wa timu za mastaa nchini Marekani (NBA All-Star Game MVP).

Mnamo 2017, mwaka ambao alishinda tuzo ya MVP ya ligi, Westbrook alikua mmoja wa wachezaji wawili katika historia ya NBA kuwa na wastani wa mara tatu-mbili kwa msimu, pamoja na Oscar Robertson mnamo 1962. Pia aliweka rekodi ya mara tatu-mbili zaidi katika msimu, akiwa nazo 42.[2] Aliendelea kuwa na wastani wa mara tatu-mbili katika misimu miwili iliyofuata na pia kuongoza ligi kwa asisti na kuwa mchezaji wa kwanza kuongoza ligi kwa pointi na asisti katika misimu mingi.[3] Mnamo 2020-2021, Westbrook alipata wastani wa mara tatu-mbili kwa mara ya nne katika misimu mitano,[4] na alimpita Robertson kwa taaluma ya mara tatu-mbili zaidi katika historia ya NBA.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Russell Westbrook kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Anderson, Sam (2017-02-01), "The Misunderstood Genius of Russell Westbrook", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-05-19 
  2. "Westbrook sets record with 42nd triple-double". ESPN.com (kwa Kiingereza). 2017-04-09. Iliwekwa mnamo 2023-05-21. 
  3. "Thunder Secure the 6-Seed, Beat Bucks 127-116 in Regular Season Finale". Daily Thunder (kwa Kiingereza). 2019-04-11. Iliwekwa mnamo 2023-05-21. 
  4. Dan Gartland (2021-05-04). "Russ Had Another Absurd Box Score-Stuffing Game". Sports Illustrated (kwa en-us). Iliwekwa mnamo 2023-05-21. 
  5. Wallace, Ava (2021-05-11), "Russell Westbrook sets triple-double record, but Wizards fall at Atlanta", Washington Post (kwa en-US), ISSN 0190-8286, iliwekwa mnamo 2023-05-21