Remmy Ongala
Remmy Ongala | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Ramadhani Mtoro Ongala |
Amezaliwa | 10 Februari, 1947 |
Asili yake | Mzaire, Mtanzania |
Amekufa | 12 Disemba, 2010 |
Kazi yake | Mwimbaji |
Ala | Sauti, Gitaa |
Miaka ya kazi | mn. 1965 - |
Ame/Wameshirikiana na | Virunga, Diblo Dibala, Orchestra Super Mazembe, Orchestra Makassy |
Remmy Ongala (10 Februari 1947 - 13 Desemba 2010) alikuwa mwanamuziki nchini Tanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alizaliwa na jina la kiraia la Ramadhani Mtoro Ongala katika jimbo la Kivu la Kongo ya Kibelgiji. Remmy alifahamika sana kwa uwezo wake wa kutungia nyimbo akiwa jukwaani. Mbali na zile anazotunga akiwa na wenziwe, lakini akiwa katika kumbi huwa anazifanyia manjonjo zaidi ya yale aliyotungia. Alikuwa mbunifu na kipenzi cha watu. Licha ya kuingia katika dini mbalimbali mwisho akaishia kuwa Mlokole hadi kifo chake.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Remmy Ongala pamoja na bendi yake ya Super Matimila, ni mashuhuri sana nchini Tanzania, na wamepiga muziki mara nyingi katika nchi za Ulaya na Marekani. Remmy Ongala kwa asili anatoka Zaire. Akiwa na umri wa miaka tisa mama yake alifariki, hivyo ikimbidi achukue jukumu la kutunza wadogo zake.
Akiwa na umri wa miaka 17, alikuwa muimbaji na mpiga ngoma katika bendi ya vijana ya Bantu Success. Hii haikuwa na maana kwa familia yake, hivyo Remmy ilimbidi atoke katika bendi. Miaka miwili baadaye, alijishughulisha tena na muziki. Alijiunga na vikundi mbalimbali vya bendi za muziki akiwa mpiga gitaa na baadhi yake zilikuwa Micky Jazz ya Zaire na Grand Mike Jazz ya huko Uganda. Mwaka 1978 alihamia Tanzania na kujiunga na bendi ya mjomba wake Ochestre Makassy ya jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1981 alijiunga na bendi ya Matimila, ikiwa na wanamuziki 18 na ikimilikiwa na mfanya biashara mmoja. Baadaye alianzisha bendi yake ya Super Matimila na kuendeleza mtindo wa kutumia magitaa 3, besi, ngoma na tarumbeta aina ya saksafoni. Remmy Ongala alipiga muziki wake kwa mtindo wa Soukous, katika maumbile mapya kabisa kwa kutumia asili na jadi ya kitanzania. Akiimba kwa kiswahili, ushairi wake mzuri una tunzi zinazohusu siasa na pia maisha ya mtu wa kawaida. Kwa ajili ya uimbaji na utunzi wake wa kuliwaza, Remmy anaitwa “Dokta” na ni mtu anayejulikana sana katika sehemu za Sinza ambazo ni jirani na anakoishi yeye na mkewe Mwingereza na watoto wao 5 na kasuku mmoja, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Albamu Alizotoa
[hariri | hariri chanzo]- 1. Songs for the Poor Man (1989)
- 2. Mambo (1992)
- 3. Sema (1995)
- 4. The Kershaw Sessions (1995)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Answers.com kuhusu Remy Ongala, maisha na kazi yake
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Remmy Ongala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |