Ravidasvir
Ravidasvir ni dawa inayotumiwa kutibu homa ya ini C (hepatitis C).[1] Kwa kawaida, hutumiwa pamoja na sofosbuvir yenye kiwango cha tiba cha 97%.[2] Dawa hii inaweza kutumika kwa watu walioambukizwa na homa ya ini C na HIV/UKIMWI [2] na inachukuliwa kwa njia ya mdomo.[1]
Madhara yake kwa ujumla ni madogo.[3] Kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, sukari ya chini ya damu inaweza kutokea.[3] Kwa wale ambao pia wana homa ya ini B (hepatitis B) kujirudia kwake kunaweza kutokea tena.[3] Dawa hii ni kizuizi cha NS5A.[4]
Ravidasvir iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Malaysia na Misri mnamo mwaka wa 2021.[2] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[5] Kuitumia kwa ajili ya matibabu kwa wiki 12 kunatarajiwa kugharimu takriban dola 300 za Marekani hadi 500.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "eEML - Electronic Essential Medicines List". list.essentialmeds.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Ravidasvir + sofosbuvir | DNDi". dndi.org. 31 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Mei 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 "24th WHO Expert Committee on Selection and Use of Essential Medicines Expert review" (PDF). WHO. WHO. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 10 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 "First hepatitis C treatment developed through South-South cooperation registered in Malaysia | DNDi". dndi.org. 14 Juni 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Aprili 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ World Health Organization (2023). The selection and use of essential medicines 2023: web annex A: World Health Organization model list of essential medicines: 23rd list (2023). Geneva: World Health Organization. hdl:10665/371090. WHO/MHP/HPS/EML/2023.02.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ravidasvir kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |