Homanyongo C

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa ugonjwa tofauti ambao wakati mwingine jina lake linachanganywa tazama Homa ya manjano

Homa ya nyongo C (Hepatitis C)
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B17.1, B18.2
ICD-9070.70,070.4, 070.5
OMIM609532
DiseasesDB5783
MedlinePlus000284
eMedicinemed/993 ped/979
MeSHD006526

Homa ya nyongo C[1] (pia homanyongo C, kwa Kiingereza Hepatitis C) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoshambulia zaidi ini.

Virusi vya Homanyongo C ndivyo vinavyosababisha ugonjwa huu wa ini. [2]

Kwa kawaida Homa ya nyongo C haionyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali, lakini ugonjwa ukiendelea unaweza ukasababisha makovu katika maini, na baada ya miaka mingi ini linapata vidonda (cirrhosis). Kwa wagonjwa wengine vidonda hivi vinaweza kusababisha ini kukosa kufanya kazi, saratani ya ini, au mishipa iliyovimba sana ya umio na tumbo, ambayo yanaweza kufanya mtu avuje damu hadi kufa.[2]

Watu wanaambukizwa virusi vya Homa ya nyongo C kwa kupitia mkondo wa damu kwa njia ya kujidunga sindano za dawa za kulevya, kutumia vifaa vichafu vya hospitali, na kuongezewa damu.

Kadri ya watu milioni 130–170 wameathirika na Homa ya nyongo C. Wataalamu walianza kuchunguza HCV katika miaka ya 1970, na walithibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo mnamo mwaka 1989.[3] Haijulikani kama ugonjwa huu unawaambukiza wanyama.

Peginterferon na ribavirin ndizo dawa pekee zinazotumika sana dhidi ya HCV. Kati ya wagonjwa asilimia 50-80 wanaotibiwa huwa wanapona. Watu wanaopata uharibifu mkubwa na kovu kwa ini (cirrhosis) au saratani ya ini wanaweza kuhitaji ini la kupandikizwa, lakini virusi huwa vinarejea baada ya kupandikiza.[4] hakuna chanjo ya kuzuia Homa ya nyongo C.

Viashiria na dalili[hariri | hariri chanzo]

Homa ya nyongo C inasababisha dalili katika wagonjwa asilimia 15 tu,[5] mara nyingi zaidi agonjwa hawaonyeshi dalili zozote.

Dalili ni kama zifuatazo: kupungua hamu ya kula, uchovu, kichefuchefu, maumivu ya viungo au misuli, kupungua uzito wa mwili.[6] Ni wagonjwa wachache ambao ni mahtuti na wanapata homa ya manjano.[7]

Kadri ya wagonjwa asilimia 10 hadi 50 wanapona bila kupata matibabu, na kati ya hao wengi ni wasichana wadogo.[7]

Uambukizo sugu[hariri | hariri chanzo]

Asilimia themanini ya watu walioambukizwa virusi wanapata madhara ya uambukizo sugu.[8] Wagonjwa wengi hawaonyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali za ugonjwa huo, [9] ingawa uambukizo sugu wa Homa ya nyongo C unasababisha uchovu.[10] Homa ya nyongo C ni chanzo kikubwa cha ini kupata vidonda pamoja na saratani ya ini kwa watu ambao wameathirika na ugonjwa huu kwa muda mrefu.[4] Kati ya asilimia 10–30 ya watu wameambukizwa baada ya miaka 30 ya kuwa na vidonda katika ini.[4][6] Pia watu wenye HomanyongoB au UKIMWI, walevi sugu, na wanaumme huwa wanapata vidonda katika ini.[6] Kwa watu wenye vidonda katika ini uwezekano wa kupata saratani ya ini ni mara ishirini zaidi ya kawaida, kiasi cha asilimia 1 hadi 3 kwa mwaka.[4][6] Kwa walevi sugu, uwezekano wa kupata ugonjwa ni mara 100 zaidi ya kawaida.[11] Homa ya nyongo C inasababisha vidonda vya ini katika asilimia 27 ya wagonjwa na inasababisha saratani ya ini kati ya asilimia 25 ya wagonjwa.[12]

Vidonda vya ini vinaweza kusababisha msukumo mkubwa wa damu katika mishipa iliyoungana na ini, kujaa maji tumboni, kuumia kirahisi au kuvuja damu, mishipa kuvimba, hasa tumboni na kwenye umio, homa ya nyongo (ngozi inakuwa ya manjano), na majeraha katika ubongo.[13]

Athari nje ya ini[hariri | hariri chanzo]

Homa ya nyongo C mara chache inasababisha ugonjwa unaojulikana kama Sjögren's syndrome (madhara dhidi ya kinga ya mwili), upungufu sio kawaida wa idadi ya blood platelets, magonjwa sugu ya ngozi, kisukari, pamoja na aina Fulani ya aina saratani ya damu iitwayo non-Hodgkin lymphomas.[14][15]

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

Virusi vya Homa ya nyongo C ni vidogo, vilivyo ndani ya kibahasha, na kiuzi kimoja, vina RNA yenye virusi.[4] Ni jamii ya hepacivirus ya familia iitwayo Flaviviridae.[10] Kuna aina saba muhimu za genotypes of HCV.[16] Nchini Marekani, genotype 1 inasababisha asilimia 70 ya magonjwa, genotype 2 inasababisha asilimia 20 ya magonjwa, na kila aina ya genotypes zingine zinasababisha asilimia 1. [6] Genotype 1 ndio inayojulikana zaidi katika nchi za Amerika ya Kusini na Ulaya.[4]

Maambukizi[hariri | hariri chanzo]

Njia ya kawaida ya uambukizaji katika nchi zilizoendelea ni kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano. Katika nchi zinazoendelea njia za kawaida za utoaji damu na utaratibu usio salama wa kimatibabu [17] Katika asilimia 20% ya wagonjwa, chanzo cha uambukizaji hakijulikani;[18] lakini vyanzo vingi vinaweza kuwa ni matumizi ya dawa ya kulevya kwa kujidunga sindano.[7]

Madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano ndiyo sababu kubwa ya kusambaza Homa ya nyongo C katika nchi nyingi duniani.[19] Uchunguzi uliofanya katika nchi 77 zimeonyesha kwamba katika nchi 25 ambayo Marekani ni mojawapo, asilimia ya watu wanaopata Homa ya nyongo C kwa kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano ni asilimia 60 hadi 80 [8] na Uchina. [19] Nchi kumi na mbili zina zaidi ya asilimia 80.[8] Zaidi ya milioni kumi ya watumizi wa madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wameambukizwa na Homa ya nyongo C; Uchina (milioni 1.6), Marekani (milioni 1.5), na Urusi(milioni 1.3) jumla ya wagonjwa walioambukizwa ni wengi sana.[8] Kiasi kikubwa cha wafungwa Marekani wana Homa ya nyongo C uwezekano wa kupata ugonjwa ni mara kumi hadi ishirini zaidi ya kiwango cha kawaida cha idadi ya watu, na utafiti umeonyesha hii inasababishwa na tabia za hatari za kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano au kujichora chale na sindano ambazo sio safi.[20][21]

Maambukizi kupitia huduma za afya[hariri | hariri chanzo]

Utoaji wa damu, mazao ya damu, na upandikizi wa viungo vya mwili bila kuchunguza HCV ndizo zinazoleta matatizo makubwa ya uambukizaji.[6] Marekani ilirasimisha uchunguzi mnamo mwaka 1992. "Tangu wakati huo kiwango cha maambukizi imepungua kuanzia kati ya mmoja kati ya 200 kwa kila kipimo cha damu[22] hadi moja kati ya 10,000 mpaka 10,000,000 kwa kila kipimo cha damu.[7][18] Kuna upungufu wa maambukizi kwa sababu kuna kipindi cha siku 11 hadi 70 ambazo ni siku ambazo mtoaji damu mtarajiwa anayepata Homa ya nyongo C na damu yao kuonyesha kwamba imeambukizwa.[18] Nchi zingine bado hazifanyi uchunguzi wa Homa ya nyongo C kwa sababu ya gharama.[12]

Mtu mwenye jeraha la sindano kutoka kwa mtu aliyeathiriwa na HCV ana uwezo wa asilimia 1.8 ya kupata ugonjwa [6] Hatari inaongezeka kama sindano inayotumika ina shimo kubwa na jeraha ni kubwa.[12] Kuna hatari kutoka kwa mfichuo wa kamasi hadi kwa damu; ingawa kiwango cha hatari hii ni ndogo, na hakuna hatari yoyote kama damu ikigusa ngozi isiyokuwa na jeraha.[12]

Vifaa vya hospitali pia vinaweza kuambukiza Homa ya nyongo C kama vile: kutumia mara kwa mara sindano na pini,mifuko ya kujaza, na vifaa visivyo visafi vya hospitali.[12] Hali mbaya ya hospitali au za kliniki za madaktari wa meno ndio sababu kubwa za maambukizi ya HCV nchini Misri, ni nchi yenye kiasi kikubwa cha maambukizi duniani.[23]

Uhusiano wa kimapenzi[hariri | hariri chanzo]

Haijulikani kama shughuli za ngono zinaweza kuleta maambukizi ya Homa ya nyongo C.[24] Ingawa kuna uhusiano kati ya njia za hatari za kufanya ngono na Homa ya nyongo C, si wazi kama maambukizi ya ugonjwa huo yanatokana na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo hayakutajwa au ngono yenyewe. [6] Ushahidi unaonyesha kwamba hakuna hatari ya maambukizi kwa wapenzi wa jinsia tofauti ambao hawana mapenzi na watu wengine.[24]

Shughuli za ngono zinazoleta viwango vya juu vya majeraha ndani ya mfereji wa mkundu, kama vile kupenyeza mkunduni, au inayotokea wakati wa maambukizo ya zinaa kama yale yanayotokea wakati wa maambukizo ya zinaa, ikiwa ni pamoja na VVU au vidonda sehemu ya siri, zote hizi zinaleta hatari ya maambukizo.[24]

Serikali ya Marekani inapendekeza matumizi ya kondomu kama njia pekee ya kuzuia maambukizi ya Homa ya nyongo C kwa watu wenye wapenzi wengi.< ref>Hepatitis C Group Education Class. United States Department of Veteran Affairs.</ref>

Kutoboa mwili[hariri | hariri chanzo]

Uchoraji wa mwili unaongeza hatari mara mbili au tatu zaidi ya kupata Homa ya nyongo C.[25] Hii inaweza kuwa kwa sababu vifaa vinavyotumiwa sio visafi au kuambukizwa na rangi iliyotumika.[25]

Uchoraji au kujitoboa mwili kama shughuli hizi zilifanywa kabla ya miaka ya kati-1980 au ilifanywa na mtu asiye na ujuzi hasa inaleta wasiwasi, kwa sababu uwezekano wa kusafisha vifaa ni ndogo sana. Hatari ya kuambukizwa inaongezeka mara mbili zaidi kama mchoro ni mkubwa.[25] Karibu nusu ya wafungwa wanatumia kwa pamoja vifaa vya kujichora ambavyo sio visafi. [25] Ni mara chache uchoraji unafanywa katika sehemu zilizosajiliwa kuambukizwa na ugonjwa wa HCV.[26]

Kugusa damu[hariri | hariri chanzo]

Vifaa vya maangalizi binafsi kama vile mashine ya kunyolea, mswaki, na mashine ya kukata kucha yanaweza kuwa na damu. Kama zikitumiwa za zaidi ya mtu mmoja uwezekano ni mkubwa wa kuambukizana HCV.[27][28] Watu wanatakiwa wawe waangalifu na mikwaruzo na vidonda au uvujaji wa damu.[28] HCV haimbukizwi kwa kushikana kama vile kukumbatiana, kupeana busu, au kula kwa pamoja au kutumia kwa pamoja vyombo vya kulia chakula.[28]

Maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto[hariri | hariri chanzo]

Maambukizi ya Homa ya nyongo C kutoka kwa mama hadi kwa mtoto hutokea kwa asilimia 10 za mimba.[29] Hakuna njia yoyote ya kupunguza hatari hii[29] wakati wa kuzaa.[18]

Hatari ya kuambukiza inaongezeka kama muda wa uchungu wa uzazi ni mrefu.[12] Hakuna ushahidi wowote unaosema mtoto akinyonyeshwa maziwa ataambukizwa HCV; lakini, mama aliyeathiriwa hatakiwi amnyonyeshe mtoto kama chuchu zake zina mpasuko au zinavuja,[30] au kama ana kiwango kikubwa cha virusi.[18]

Uchunguzi wa ugonjwa[hariri | hariri chanzo]

Serologic profile of Homa ya nyongo C infection

Uchunguzi wa Homa ya nyongo C unaangalia yafuatayo: HCV kingamwili, ELISA, Western blot, pamoja na idadi ya HCV RNA.[6] Polymerase chain reaction (PCR) inagundua HCV RNA wiki mmoja au mbili baada ya kuambukizwa, wakati vikinga mwili huchukua muda mrefu kutengenezwa na kuonekana.[13]

Maambukizo ya muda mrefu ya Homa ya nyongo C, yanayoletwa na virusi vya Homa ya nyongo C ambavyo vinaweza kuishi mwilini kwa muda unaoweza kuzidi miezi sita kama RNA ipo au haipo.[9] Kwa sababu ugonjwa huu kali hauonyeshi dalili zozote kwa muda mrefu,[9] madaktari huwa kwa kawaida wanagudua ugonjwa huu wanapofanya uchunguzi wa maini au wakati wanapofanya utaratibu wa kawaida wa kuchunguza afya za watu walio hatarini. Uchunguzi hauwezi kutofautisha kati ya ugonjwa mahututi na ugonjwa sugu wa maini.[12]

Upimaji damu[hariri | hariri chanzo]

Upimaji wa Homa ya nyongo C kwa kawaida huanza na vipimo vya damu ili kugundua uwepo wa kingamwili kwa HCV kwa kutumia kimeng'enya immunoassay.[6] Kama upimaji huu ni chanya, kipimo cha itafanywa ili kuthibitisha immunoassay na kuamua ukali.[6] Uchanganuzi wa recombinant immunoblot inathibitisha immunoassay, na mmenyuko wa HCV RNA polimeresi huamua ukali.[6] Kama hakuna RNA na immunoblot ni chanya, mtu alikuwa na maambukizi ya awali lakini ikaisha na aidha kwa matibabu au yenyewe; kama immunoblot ni hasi, immunoassay ilikuwa na makosa.[6] Inachukua wiki sita hadi nane kwa kufuatia maambukizi kabla ya vipimo vya immunoassay kuonekana kuwa yako.[10]

Vimeng'enya vya ini hubadilika wakati wa sehemu ya awali ya maambukizi;[9] kwa wastani huanza kupanda katika wiki ya saba baada ya kuambukizwa.[10] Ini za vimeng'enya huhusiana vibaya na ukali wa ugonjwa.[10]

Biopsi[hariri | hariri chanzo]

Biopsi za ini zinaweza kuamua kiwango cha uharibifu wa ini, lakini kuna hatari kutokana na utaratibu huo.[4] Mabadiliko ya kawaida biopsi hutambua ni lymphocytes ndani ya tishu ya ini, vinyeleo vya limfu katika triad portal, na mabadiliko kwa vichirizi vya nyongo.[4] Kuna idadi ya vipimo vya damu vinavyopatikana ambavyo vinajaribu kuamua kiwango cha uharibifu na kupunguza haja ya biopsi.[4]

Uchunguzi[hariri | hariri chanzo]

Watu wachache, kama asilimia 5-50 walioambukizwa nchini Marekani na Canada, wanafahamu hali yao.[25] Kupima inapendekezwa kwa watu walio na hatari ya juu, ambao ni pamoja na watu wenye chale .[25] Uchunguzi pia inapendekezwa kwa watu wenye muinuko wa kimeng'enya ya ini kwani hii ni ishara ya pekee ya homanyongosugu ya mara kwa mara.[31] Uchunguzi wa mara kwa mara hapendekezwi nchini Marekani.[6]

Kinga[hariri | hariri chanzo]

Kufikia mwaka 2011, hakuna chanjo iliyopatikana kwa homa ya nyongo C. Chanjo zinatengenezwa, na baadhi zimeonyesha matokeo ya kutia moyo.[32] Mchanganyiko wa mikakati ya kuzuia, kama vile mipango ya kubadilishana sindano na matibabu ya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, hupunguza hatari ya homa ya nyongo C katika watumiaji wa madawa ya kujindunga kwa mishipa kwa karibu asilimia 75.[33] Kuwachunguza watoaji damu ni muhimu katika kiwango cha kitaifa, kama ni kufuata tahadhari za ulimwenguni ndani ya vituo vya afya.[10] Katika nchi ambako kuna ugavi usiotosha wa sindano hasi, watoa huduma wanapaswa kupeana madawa kwa mdomo badala ya kupitia sindano.[12]

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

HCV inasababisha maambukizi sugu katika asilimia 50-80 ya watu walioambukizwa. Takriban asilimia 40-80 ya kesi hizi humalizika kwa matibabu.[34][35]

Katika matukio machache, maambukizi yanaweza kuisha bila ya tiba.[7] Watu wenye homa ya nyongo C sugu ni lazima wajiepushe pombe na madawa yaa sumu kwa ini,[6] na wanapaswa kupatiwa chanjo ya homa y a manjano A na homanyongoB [6] Watu walio na cirrhosis wanapaswa kuwa na vipimo vya ultrasound vya saratani ya ini.[6]

Madawa[hariri | hariri chanzo]

Watu wenye maambukizi ya ini ya HCV yaliyothibitika yasiyo ya kawaida wanapaswa kutafuta matibabu. [6] Matibabu ya sasa ni mchanganyiko wa pegylated interferon na madawa ya kupunguza makali ya ukimwi ribavirin kwa muda wa wiki 24 au 48, kulingana na aina ya HCV .[6] Matokeo bora hutokea kwa asilimia 50-60% ya watu waliotibiwa. [6] Kuchanganya ama boceprevir au telaprevir na ribavirin na peginterferon alfa inaboresha matokeo ya homa ya nyongo C genotype 1.[36][37][38] Madhara kwa matibabu ni ya kawaida, nusu ya watu wanaotibiwa hupata dalili kama homa ya mafua, na theluthi ya watu hupata matatizo ya mhemuko.[6] Tiba katika miezi sita za kwanza ni bora zaidi kuliko baada ya homa ya nyongo C kuwa sugu.[13] Kama mtu anapata maambukizi mapya na haijaisha baada ya wiki nane hadi kumi na mbili, wiki 24 ya pegylated interferon inapendekezwa.[13] Kwa watu wenye thalasemia (ugonjwa wa damu), ribavirin inaonekana kuwa muhimu, lakini huongeza haja ya upaji wa damu.[39]

Watetezi wanadai tiba kadhaa mbadala kuwa na manufaa kwa homa ya nyongo C ikiwa ni pamoja na maziwa mbigili, ginseng, na colloidal silver [40] Hata hivyo, hakuna tiba mbadala imeonekana kuboresha matokeo katika homa manjano C, na hakuna ushahidi upo ambao tiba mbadala ina athari yoyote kwenye virusi wakati wote .[40][41][42]

Ubashiri[hariri | hariri chanzo]

Majibu ya matibabu hutofautiana kulingana na genotype. Majibu endelevu ni kadiri asilimia 40-50 kwa watu wenye HCV genotype 1 kwa muda wa wiki 48 ya matibabu.[4] Majibu endelevu hutokea katika asilimia 70-80 kwa watu walio na genotypes HCV 2 na 3 kwa muda wa wiki 24 ya matibabu.[4] Majibu endelevu ni kadiri ya asilimia 65 kwa watu wenye genotype 4 kwa muda wa wiki 48 ya matibabu. Ushahidi wa matibabu katika ugonjwa genotype 6 kwa sasa ni chache, na ushahidi uliopo ni wa muda wa wiki 48 ya tiba katika vipimo sawa na ugonjwa wa genotype 1.[43]

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Maambukizi ya homa ya nyongo C duniani kote mwaka 1999
Disability-adjusted life year ya homa ya nyongo C mwaka 2004 kwa kila wakazi 100,000
     no data      <10      10-15      15-20      20-25      25-30      30-35
     35-40      40-45      45-50      50-75      75–100      >100

Kati ya watu milioni 130 na 170, au ~ asilimia 3 ya idadi ya watu duniani, wanaishi na homa ya nyongo C sugu.[44] Kati ya watu milioni 3-4 huambukizwa kwa mwaka, na zaidi ya watu 350,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa-husiana na homa ya nyongo C.[44] Viwango vimeongezeka pakubwa katika karne ya 20 kutokana na mchanganyiko wa IDU na madawa ya kujidunga katika mishipa au vifaa vya matibabu visivyokifishwa.[12]

Nchini Marekani, kadiri ya asilimia 2 ya watu wana homa ya nyongo C,[6] pamoja na kesi mpya 35,000 hadi 185,000 kwa mwaka. Viwango vimepungua katika nchi za Magharibi tangu miaka ya 1990 kutokana na uchunguzi wa kuboresha damu kabla ya utoaji.[13] Vifo vya kila mwaka kutokana na HCV nchini Marekani ni kadiri kutoka 8,000 hadi 10,000. Matarajio ni kwamba kiwango hiki cha vifo itaongezeka wakati watu walioathirika kwa utoaji damu kabla ya kupimwa HCV kuwa wagonjwa na kufa.[45]

Viwango vya maambukizi viko juu katika baadhi ya nchi za Afrika na Asia.[46] Nchi zilizi na viwango vya juu sana vya maambukizi ni Misri (asilimia 22), Pakistani (asilimia 4.8) na Uchina (asilimia 3.2).[44] Kiwango cha juu nchini Misri inahusishwa na kampeni ya umma ya matibabu ya sasa-iliyositishwa ya schistosomiasis, kwa kutumia sindano za kioo zisizokifishwa vizuri.[12]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya 1970 katikati, Harvey J. Alter, Mkuu wa Sehemu ya Magonjwa ya Maambukizi katika Idara ya Madawa ya Kujidunga kwa mishii katika Taasisi ya Kitaifa ya Afya, na timu yake ya utafiti walionyesha kuwa kesi nyingi za utoaji wa baada-damu ya homanyongohazikutokana na viruzi vya homanyongoA au B. Licha ya ugunduzi huu, jitihada za utafiti wa kimataifa za kutambua virusi zilishindiana kwa miaka kumi ifuatayo. Mwaka 1987, Michael Houghton, qui-Lim Choo, na George Kuo katika Shirika la Chiron, wakishirikiana na Dkt. DW Bradley kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, walitumia mbinu mpya ya molecular cloning ya kubaini kiumbe kisichojulikana na kukuza uchunguzi wa ubainishaji..[47] Mwaka 1988, Alter alithibitisha virusi kwa kuthibitisha uwepo wao katika jopo la vielelezo vya homanyongozisizo A zisizo B. Mwezi Aprili 1989, ugunduzi wa HCV ulichapishwa katika makala mbili katika jarida la "Sayansi".[48][49] Ugunduzi ulisababisha mafanikio makubwa katika utambuzi na kuboresha matibabu ya kupunguza makali ya virusi.[47] Mwaka 2000, Dkt. Alter na Houghton walitukuzwa na Tuzo ya Lasker ya Utafiti wa Kitabibu ya Hospitali ya "kuongoza kazi inayosababisha ugunduzi wa virusi vinavyosababisha homa ya nyongo C na mbinu za kukuza uchunguzi ambazo zilipunguza hatari ya utoaji damu-ilihusisha homa y a manjano nchini Marekani kutoka asilimia 30 mwaka 1970 hadi karibu sifuri mwaka 2000."[50]

Chiron aliwasilisha hataza kadhaa kuhusu virusi na uchunguzi wake.[51] Maombi ya mashindano ya hataza na CDC ilikuwa imeshuka mwaka 1990 baada ya Chiron kulipa dola milioni 1,900,000 kwa CDC na dola 337,500 kwa Bradley. Mwaka 1994, Bradley alimshtaki Chiron, wakitaka kubatilisha hataza, alitaka yeye mwenyewe ajumuishwe kama mbunifu mshiriki, na kupokea mapato ya uharibifu na ya mrahaba. Alisitisha mashtaka mwaka 1998 baada ya kupoteza mbele ya mahakama ya rufaa.[52]

Jamii na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Mwungano wa Dunia wa Homanyongo inaratibu siku ya Dunia ya Homa ya nyongo, hufanyika kila mwaka tarehe 28 mwezi Julai.[53] Gharama za kiuchumi za homa ya nyongo C ni muhimu kwa mtu binafsi na kwa jamii kijumla. Nchini Marekani wastani ya gharama ya maisha ya ugonjwa huo ilikadiriwa kuwa dola 33,407 za marekani mwaka 2003,[54] na gharama ya kupandikiza ini ni takriban dola 200,000 za Marekani kufikia mwaka 2011.[55] Nchini Canada gharama ya matibabu ya kupambana na virusi yalikuwa juu kama dola 30,000 za Canada mwaka 2003,[56] wakati Marekani gharama ni kati ya dola 9200 na 17,600 za Marekani mwaka 1998.[54] Katika maeneo mengi ya dunia watu wanashindwa kumudu matibabu na madawa ya kupunguza makali ya virusi kwa sababu ya kukosa bima au bima waliyo nayo haitalipa madawa ya kupunguza makali ya virusi.[57]

Utafiti[hariri | hariri chanzo]

Kufikia mwaka 2011, karibu madawa mia moja yanakuzwa kwa ajili ya homa ya nyongo C.[55] Dawa hizi ni pamoja na chanjo za kutibu homa ya manjano, immunomodulators, na vizuia vya cyclophilin.[58] Uwezekano wa matibabu haya mapya yamekuja kutokana na uelewa mzuri wa virusi vya homa ya nyongo C.[59]

References[hariri | hariri chanzo]

 1. Wakati mwingine homa ya nyongo inaitwa "homa ya manjano" lakini hii ni ugonjwa tofauti. Taz homa ya manjano (ing. Yellow fever)
 2. 2.0 2.1 (2004) in Ryan KJ, Ray CG (editors): Sherris Medical Microbiology, 4th, McGraw Hill, 551–2. ISBN 0838585299. 
 3. Houghton M (Novemba 2009). "The long and winding road leading to the identification of the hepatitis C virus". Journal of Hepatology 51 (5): 939–48. doi:10.1016/j.jhep.2009.08.004 . PMID 19781804 .
 4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 Rosen, HR (2011-06-23). "Clinical practice. Chronic hepatitis C infection.". The New England journal of medicine 364 (25): 2429–38. PMID 21696309 . http://www.casemedicine.com/ambulatory/Continuity%20Clinic/Clinic%20Articles/1)%20July/2)Week%20of%20July%2025th/chronic%20hep%20c.NEJM.pdf. Retrieved 2012-10-05.
 5. Maheshwari, A; Ray, S, Thuluvath, PJ (2008-07-26). "Acute hepatitis C.". Lancet 372 (9635): 321–32. doi:10.1016/S0140-6736(08)61116-2 . PMID 18657711 .
 6. 6.00 6.01 6.02 6.03 6.04 6.05 6.06 6.07 6.08 6.09 6.10 6.11 6.12 6.13 6.14 6.15 6.16 6.17 6.18 6.19 6.20 6.21 Wilkins, T; Malcolm, JK, Raina, D, Schade, RR (2010-06-01). "Hepatitis C: diagnosis and treatment.". American family physician 81 (11): 1351–7. PMID 20521755 . http://www.aafp.org/afp/2010/0601/p1351.html.
 7. 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 (2011) Chronic Hepatitis C Virus Advances in Treatment, Promise for the Future.. Springer Verlag, 4. ISBN 9781461411918. 
 8. 8.0 8.1 8.2 8.3 Nelson, PK; Mathers, BM, Cowie, B, Hagan, H, Des Jarlais, D, Horyniak, D, Degenhardt, L (2011-08-13). "Global epidemiology of hepatitis B and hepatitis C in people who inject drugs: results of systematic reviews.". Lancet 378 (9791): 571–83. doi:10.1016/S0140-6736(11)61097-0 . PMID 21802134 .
 9. 9.0 9.1 9.2 9.3 (2011) Chronic Hepatitis C Virus Advances in Treatment, Promise for the Future.. Springer Verlag, 103–104. ISBN 9781461411918. 
 10. 10.0 10.1 10.2 10.3 10.4 10.5 Dolin, [edited by] Gerald L. Mandell, John E. Bennett, Raphael (2010). Mandell, Douglas, and Bennett's principles and practice of infectious diseases, 7th ed., Philadelphia, PA: Churchill Livingstone/Elsevier, Chapter 154. ISBN 978-0443068393. 
 11. Mueller, S; Millonig, G, Seitz, HK (2009-07-28). "Alcoholic liver disease and hepatitis C: a frequently underestimated combination.". World journal of gastroenterology : WJG 15 (28): 3462–71. PMID 19630099 .
 12. 12.00 12.01 12.02 12.03 12.04 12.05 12.06 12.07 12.08 12.09 Alter, MJ (2007-05-07). "Epidemiology of hepatitis C virus infection.". World journal of gastroenterology : WJG 13 (17): 2436–41. PMID 17552026 .
 13. 13.0 13.1 13.2 13.3 13.4 Ozaras, R; Tahan, V (2009 Apr). "Acute Homa ya nyongo C: prevention and treatment.". Expert review of anti-infective therapy 7 (3): 351–61. PMID 19344247 .
 14. Zignego AL, Ferri C, Pileri SA, Caini P, Bianchi FB (Januari 2007). "Extrahepatic manifestations of Hepatitis C Virus infection: a general overview and guidelines for a clinical approach". Digestive and Liver Disease 39 (1): 2–17. doi:10.1016/j.dld.2006.06.008 . PMID 16884964 .
 15. Louie, KS; Micallef, JM, Pimenta, JM, Forssen, UM (2011 Jan). "Prevalence of thrombocytopenia among patients with chronic hepatitis C: a systematic review.". Journal of viral hepatitis 18 (1): 1–7. PMID 20796208 .
 16. Nakano T, Lau GM, Lau GM, Sugiyama M, Mizokami M (Desemba 2011). "An updated analysis of hepatitis C virus genotypes and subtypes based on the complete coding region". Liver Int.. doi:10.1111/j.1478-3231.2011.02684.x . PMID 22142261 .
 17. Maheshwari, A; Thuluvath, PJ (2010 Feb). "Management of acute Homa ya nyongo C.". Clinics in liver disease 14 (1): 169–76; x. PMID 20123448 .
 18. 18.0 18.1 18.2 18.3 18.4 Pondé, RA; Mikhaĭlova, A (2011 Feb). "Hidden hazards of HCV transmission.". Medical microbiology and immunology 200 (1): 7–11. PMID 20461405 .
 19. 19.0 19.1 Xia, X; Luo, J, Bai, J, Yu, R (2008 Oct). "Epidemiology of HCV infection among injection drug users in China: systematic review and meta-analysis.". Public health 122 (10): 990–1003. doi:10.1016/j.puhe.2008.01.014 . PMID 18486955 . https://archive.org/details/sim_public-health_2008-10_122_10/page/990.
 20. Imperial, JC (2010 Jun). "Chronic hepatitis C in the state prison system: insights into the problems and possible solutions.". Expert review of gastroenterology & hepatology 4 (3): 355–64. PMID 20528122 .
 21. Vescio, MF; Longo, B, Babudieri, S, Starnini, G, Carbonara, S, Rezza, G, Monarca, R (2008 Apr). "Correlates of hepatitis C virus seropositivity in prison inmates: a meta-analysis.". Journal of epidemiology and community health 62 (4): 305–13. PMID 18339822 .
 22. Marx, John (2010). Rosen's emergency medicine: concepts and clinical practice 7th edition. Philadelphia, PA: Mosby/Elsevier, 1154. ISBN 9780323054720. 
 23. Highest Rates of Hepatitis C Virus Transmission Found in Egypt. Al Bawaba (2010-08-09). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-05-15. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.
 24. 24.0 24.1 24.2 Tohme RA, Holmberg SD (Juni 2010). "Is sexual contact a major mode of hepatitis C virus transmission?". Hepatology 52 (4): 1497–505. doi:10.1002/hep.23808 . PMID 20635398 .
 25. 25.0 25.1 25.2 25.3 25.4 25.5 Jafari, S; Copes, R, Baharlou, S, Etminan, M, Buxton, J (2010 Nov). "Tattooing and the risk of transmission of hepatitis C: a systematic review and meta-analysis.". International journal of infectious diseases : IJID : official publication of the International Society for Infectious Diseases 14 (11): e928-40. PMID 20678951 . http://natap.org/2010/HCV/tatoohcv.pdf.
 26. Hepatitis C. Center for Disease Control and Prevention. Iliwekwa mnamo 2 Januari 2012.
 27. Lock G, Dirscherl M, Obermeier F, et al. (Septemba 2006). "Hepatitis C —contamination of toothbrushes: myth or reality?". J. Viral Hepat. 13 (9): 571–3. doi:10.1111/j.1365-2893.2006.00735.x . PMID 16907842 .
 28. 28.0 28.1 28.2 Hepatitis C. FAQ – CDC Viral Hepatitis. Iliwekwa mnamo 2 Jan 2012.
 29. 29.0 29.1 Lam, NC; Gotsch, PB, Langan, RC (2010-11-15). "Caring for pregnant women and newborns with hepatitis B or C.". American family physician 82 (10): 1225–9. PMID 21121533 .
 30. Mast EE (2004). "Mother-to-infant hepatitis C virus transmission and breastfeeding". Advances in Experimental Medicine and Biology 554: 211–6. PMID 15384578 .
 31. Senadhi, V (2011 Jul). "A paradigm shift in the outpatient approach to liver function tests.". Southern medical journal 104 (7): 521–5. PMID 21886053 . https://archive.org/details/sim_southern-medical-journal_2011-07_104_7/page/521.
 32. Halliday, J; Klenerman, P, Barnes, E (2011 Mei). "Vaccination for hepatitis C virus: closing in on an evasive target.". Expert review of vaccines 10 (5): 659–72. doi:10.1586/erv.11.55 . PMID 21604986 .
 33. Hagan, H; Pouget, ER, Des Jarlais, DC (2011-07-01). "A systematic review and meta-analysis of interventions to prevent hepatitis C virus infection in people who inject drugs.". The Journal of infectious diseases 204 (1): 74–83. PMID 21628661 .
 34. Torresi, J; Johnson, D, Wedemeyer, H (2011 Jun). "Progress in the development of preventive and therapeutic vaccines for hepatitis C virus.". Journal of hepatology 54 (6): 1273–85. doi:10.1016/j.jhep.2010.09.040 . PMID 21236312 .
 35. Ilyas, JA; Vierling, JM (2011 Aug). "An overview of emerging therapies for the treatment of chronic hepatitis C.". Clinics in liver disease 15 (3): 515–36. PMID 21867934 .
 36. Foote BS, Spooner LM, Belliveau PP (Septemba 2011). "Boceprevir: a protease inhibitor for the treatment of chronic hepatitis C". Ann Pharmacother 45 (9): 1085–93. doi:10.1345/aph.1P744 . PMID 21828346 . https://archive.org/details/sim_annals-of-pharmacotherapy_2011-09_45_9/page/1085.
 37. Smith LS, Nelson M, Naik S, Woten J (Mei 2011). "Telaprevir: an NS3/4A protease inhibitor for the treatment of chronic hepatitis C". Ann Pharmacother 45 (5): 639–48. doi:10.1345/aph.1P430 . PMID 21558488 . https://archive.org/details/sim_annals-of-pharmacotherapy_2011-05_45_5/page/639.
 38. Ghany MG, Nelson DR, Strader DB, Thomas DL, Seeff LB (Oktoba 2011). "An update on treatment of genotype 1 chronic hepatitis C virus infection: 2011 practice guideline by the American Association for the Study of Liver Diseases". Hepatology 54 (4): 1433–44. doi:10.1002/hep.24641 . PMC 3229841 . PMID 21898493 .
 39. Alavian SM, Tabatabaei SV (Aprili 2010). "Treatment of chronic hepatitis C in polytransfused thalassaemic patients: a meta-analysis". J. Viral Hepat. 17 (4): 236–44. doi:10.1111/j.1365-2893.2009.01170.x . PMID 19638104 .
 40. 40.0 40.1 Hepatitis C and CAM: What the Science Says Archived 13 Mei 2013 at the Wayback Machine.. NCCAM Machi 2011. (Retrieved 7 Machi 2011)
 41. Liu, J; Manheimer, E, Tsutani, K, Gluud, C (2003 Mar). "Medicinal herbs for hepatitis C virus infection: a Cochrane hepatobiliary systematic review of randomized trials.". The American journal of gastroenterology 98 (3): 538–44. PMID 12650784 . https://archive.org/details/sim_american-journal-of-gastroenterology_2003-03_98_3/page/538.
 42. Rambaldi, A; Jacobs, BP, Gluud, C (2007-10-17). "Milk thistle for alcoholic and/or hepatitis B or C virus liver diseases.". Cochrane database of systematic reviews (Online) (4): CD003620. PMID 17943794 .
 43. Fung J, Lai CL, Hung I, et al. (Septemba 2008). "Chronic hepatitis C virus genotype 6 infection: response to pegylated interferon and ribavirin". The Journal of Infectious Diseases 198 (6): 808–12. doi:10.1086/591252 . PMID 18657036 .
 44. 44.0 44.1 44.2 WHO Hepatitis C factsheet (2011). Iliwekwa mnamo 2011-07-13.
 45. Colacino, ed. by J. M.; Heinz, B. A. (2004). Hepatitis prevention and treatment. Basel: Birkhäuser, 32. ISBN 9783764359560. 
 46. al.], edited by Gary W. Brunette ... [et. CDC health information for international travel : the Yellow Book 2012. New York: Oxford University, 231. ISBN 9780199769018. 
 47. 47.0 47.1 Boyer, JL (2001). Liver cirrhosis and its development: proceedings of the Falk Symposium 115. Springer, 344. ISBN 9780792387602. 
 48. Choo QL, Kuo G, Weiner AJ, Overby LR, Bradley DW, Houghton M (Aprili 1989). "Isolation of a cDNA clone derived from a blood-borne non-A, non-B viral hepatitis genome". Science 244 (4902): 359–62. doi:10.1126/science.2523562 . PMID 2523562 .
 49. Kuo G, Choo QL, Alter HJ, et al. (Aprili 1989). "An assay for circulating antibodies to a major etiologic virus of human non-A, non-B hepatitis". Science 244 (4902): 362–4. doi:10.1126/science.2496467 . PMID 2496467 .
 50. Winners Albert Lasker Award for Clinical Medical Research, The Lasker Foundation. Retrieved 20 Februari 2008.
 51. Houghton, M., Q.-L. Choo, and G. Kuo. NANBV Diagnostics and Vaccines. European Patent No. EP-0-3 18-216-A1. European Patent Office (filed 18 Novemba 1988, published 31 Mei 1989).
 52. Wilken, Judge. United States Court of Appeals for the Federal Circuit. United States Court of Appeals for the Federal Circuit. Iliwekwa mnamo 11 Januari 2012.
 53. Eurosurveillance editorial, team (2011-07-28). "World Hepatitis Day 2011.". Euro surveillance : bulletin europeen sur les maladies transmissibles = European communicable disease bulletin 16 (30). PMID 21813077 .
 54. 54.0 54.1 Wong, JB (2006). "Hepatitis C: cost of illness and considerations for the economic evaluation of antiviral therapies.". PharmacoEconomics 24 (7): 661–72. PMID 16802842 .
 55. 55.0 55.1 El Khoury, A. C.; Klimack, W. K., Wallace, C., Razavi, H. (1 Desemba 2011). "Economic burden of hepatitis C-associated diseases in the United States". Journal of Viral Hepatitis. doi:10.1111/j.1365-2893.2011.01563.x .
 56. Hepatitis C Prevention, Support and Research ProgramHealth Canada. Public Health Agency of Canada (Nov 2003). Iliwekwa mnamo 10 Januari 2012.
 57. Zuckerman, edited by Howard Thomas, Stanley Lemon, Arie (2008). Viral Hepatitis., 3rd ed., Oxford: John Wiley & Sons, 532. ISBN 9781405143882. 
 58. Ahn, J; Flamm, SL (2011 Aug). "Hepatitis C therapy: other players in the game". Clinics in liver disease 15 (3): 641–56. doi:10.1016/j.cld.2011.05.008 . PMID 21867942 .
 59. Vermehren, J; Sarrazin, C (2011 Feb). "New HCV therapies on the horizon.". Clinical microbiology and infection : the official publication of the European Society of Clinical Microbiology and Infectious Diseases 17 (2): 122–34. PMID 21087349 .