Raúl Correia Mendes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Raúl Augusto Leiro Correia Mendes
Amekufa 2015
Nchi Angola
Majina mengine Raul
Kazi yake Mwandishi wa Habari na mtengeneza filam

Raúl Augusto Leiro Correia Mendes (Luanda, 3 Septemba 1949 - Luanda, Machi 2015) alikuwa mwandishi wa habari na mtengenezaji wa filamu wa Angola. [1] Alifanya kazi huko Televisão Pública de Angola (TPA) akiwa kama mpiga picha, mhariri, mtayarishaji na mkurugenzi. [2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Raúl Correia Mendes alianza taaluma yake kama mtayarishaji wa Runinga huko TVA mnamo mwaka 1972, akifanya kazi kwenye michezo, muziki na vipindi vya habari. Mnamo mwaka 1974 alijiunga na Televisão Pública de Angola, na alikuwa sehemu ya timu ambayo ilifanya rasmi matangazo ya kwanza ya televisheni nchini Angola. [2]

Alipofariki Waziri wa Mawasiliano ya Jamii wa Angola, José Luís de Matos, alitoa taarifa kwa umma katika kumbukumbu yake. [2]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

 • Algodão, 1977
 • Sahara a coragem vem no vento. Short documentary, 1977.
 • Bom Dia Camarada, 1978
 • O Ouro branco de Angola, 1978
 • Louanda Luanda, 1980
 • O Encontro, 1980
 • O Legado do Gigante, 1980
 • A Nossa Musica, 1980
 • Kitala, 1982
 • Jidanti Jimba, 1982

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. FESPACO; L'Association des Trois Mondes (2000). "Correia Mendes, Raul". Les cinémas d'Afrique: dictionnaire. KARTHALA Editions. uk. 135. ISBN 978-2-84586-060-5. 
 2. 2.0 2.1 2.2 Angola: Ministro da Comunicação Social consternado com morte de Jornalista da TPA Archived 9 Oktoba 2020 at the Wayback Machine., 16 March 2015.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Raúl Correia Mendes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.