RC Celta de Vigo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Raisi wa timu ya RC Celta de Vigo, Carlos Mouriño

RC Celta de Vigo (inajulikana kama Celta Vigo au Celta tu) ni klabu ya soka ya Hispania iliyoko, Vigo, Galisia. Kwa sasa timu yake inacheza La Liga.

Timu iliundwa 23 Agosti 1923 kutokana na muungano kati ya Real Vigo Sporting na Real Fortuna FC. Jina la utani Os Celestes, linatokana na kwamba wanacheza wakiwa wamevaa jezi za anga la bluu na soksi pamoja na kaptula nyeupe.

Uwanja wa nyumbani unaitwa Abanca-Balaídos ambao wanakaa watazamaji 29,000. Jina la Celta linatokana na Wakelti ambao walikuwapo kwenye mkoa huo. Mpinzani wake mkuu ni klabu ya Kigalisia Deportivo de La Coruña, ambaye hushindana na derby wa Kigalisia.

Celta haijawahi kushinda ligi wala Copa del Rey, ingawa wamefika fainali mara tatu. Moja ya misimu bora ya timu ulikuwa 1970-1971, walipomaliza bila kufungwa mchezo nyumbani na walijulikana kama "wauaji wakuu". Celta alimaliza wa sita na alipata nafasi kwenye Kombe la UEFA kwa mara ya kwanza.

Klabu hiyo ilikamilisha nafasi yao bora ya kuwa wanne mwaka 2002-03, na kupata nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ya 2003-04 , ambapo waliondolewa na Arsenal katika mzunguko wa 16. Katika 2016-2017 UEFA Europa League, Celta ilifikia nusu fainali za UEFA Europa League kwa mara ya kwanza, na kupoteza kwa Manchester United.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu RC Celta de Vigo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.