Ghom

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Qom)
Msikiti wa kaburi la Fatima bint Masumeh mjini Ghom

Ghom (pia Qom, Qum au Kum, kwa Kifarsi قم) ni makao makuu ya mkoa wa Ghom nchini Iran yenye wakazi 1,292,000. Unahesabiwa kuwa moja ya miji mitakatifu ya Washia.

Iko takriban kilomita 130 upande wa kusini wa Tehran kwenye njia ya kuelekea Isfahan.

Msingi wa umuhimu wa kidini ni kaburi la Fatima Masumeh, aliyekuwa binti wa imamu wa saba wa Washia na dada wa Imam Reza anayeheshimiwa kama imamu wa nane wa Washia.

Leo hii Ghom ni mashuhuri hasa kama kitovu cha elimu ya Kishia; tangu karne ya 19 seminari za kusomesha ulama zilipanuliwa na leo hii ni mahali ambako ulama wengi wa Iran wanasoma.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ghom kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.