Qin Shi Huang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Qin Shi Huang.
Ufalme wa Qin Shi Huang wakati wa kifo chake

Qin Shi Huang (pia: Qin Shi Huangdi) alikuwa Kaisari wa kwanza wa China.

Alizaliwa mwaka 259 KK kama mtoto wa mfalme wa dola moja kati ya falme 7 zilizoshindana juu ya kipaumbele ndani ya China.

Alirithi ufalme wa Qin mwaka 247 KK alipokuwa na umri wa miaka 13. Kwa njia ya vita alishinda falme zote nyingine za China akaunganisha China yote mara ya kwanza.

Msingi wa utawala wake ulikuwa sheria zake zilizotangazwa kote. Kila jaribio la kuepukana au kuvunja sheria hizi liliadhibiwa vikali.

Qin Shi Huang alianzisha miradi mingi mikubwa. Alianzisha ujenzi wa ukuta mkubwa wa China kama kizuizi dhidi ya mashambulio wa makabila kutoka kaskazini. Alijaribu kuunganisha ufalme wake mkubwa kwa kujenga barabara nyingi. Aliandaa kaburi lake kubwa lililokuwa na eneo kama mji na ndani yake aliweka askari za udongo wa ufinyanzi wa kuchomwa maelfu kama walinzi.

Kwa shughuli hizi zote lakhi za watu walipaswa kufanya kazi wengi walikufa na waliojaribu kujificha walinyongwa. Kaisari alichukia mafundisho ya Ukonfusio akaua wataalamu wake na kuchoma vitabu.

Kwa upande wa utamaduni na utawala alisanifishwa mwandiko wa Kichina

Wiki crown-template.png Makala hii kuhusu Kaizari fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Qin Shi Huang kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.