Nge-bila-mkia
Nge-bila-mkia | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Aina ya nge-vitabu (Chelifer cancroides) akionyesha magando yake
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 6 za juu: |
Nge-bila-mkia ni arithropodi wa oda Pseudoscorpiones katika ngeli Arachnida. Kinyume na nge wa kawaida wadudu hawa hawana mkia, kwa hivyo jina lao. Ukubwa wao ni mdogo sana: mm 2-8; spishi kubwa kabisa (Garypus titanius) ina mm 12 tu. Wanatokea mahali popote ambapo wanaweza kukamata wadudu wadogo: chini ya gamba la miti, katika takataka za majani, katika ardhi, chini ya mawe, katika nyufa za miamba, katika mapango na katika pwaji ya ufuko. Kama arakinida wote wana miguu minane. Pedipalpi zao zinafanana na zile za nge zenye magando ambayo yana kidole kinachoweza kusogea. Kidole hiki kina tezi ya sumu inayoingizwa katika mawindo. Maji ya umeng'enyaji yakamuliwa kwa windo na baada ya kumeng'enya chakula myeyuko ufyondwa. Nge-bila-mkia wanaweza kusokota hariri kama buibui lakini matezi hayapo katika mwisho wa fumbatio lakini katika kelisera (chelicerae). Kwa hariri hii hutengeneza kifukofuko kwa umbo wa sahani kinachotumika kwa kupandana, kuambua au kungoja mwisho wa hali ya hewa baridi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ayyalonia dimentmani (Chthoniidae)
-
Chelifer cancroides (Cheliferidae)
-
Lamprochernes sp. akibebwa na Leptopeza flavipes (foresia)
-
Neobisium sylvaticum (Neobisiidae)
-
Neopseudogarypus scutellatus (Pseudogarypidae)
-
Lusoblothrus aenigmaticus (Syarinidae)