Chatimwamba
Mandhari
(Elekezwa kutoka Pseudocossyphus)
Chatimwamba | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Chatimwamba ni ndege wa jenasi Monticola katika familia Muscicapidae. Spishi kadhaa ziliainishwa katika jenasi Pseudocossyphus.
Ndege hawa wana mgongo kahawia, mweusi au buluu, kichwa buluu, buluukijivu au kijivu na tumbo jekundu. Wanatokea Afrika na Asia. Kwa kawaida huonekana juu ya miwamba, majabali na vilima vya mawe. Hula wadudu, watambaachi wadogo na beri. Hujenga tago lao kwa vitu vyororo kama sufu, manyoya na nyuzinyuzi juu ya uoto mfupi, katika ufa wa mwamba au kati ya mawe. Jike huyataga mayai 2-5.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Monticola angolensis, Chatimwamba-miyombo (Miombo Rock Thrush)
- Monticola bensoni, Chatimwamba wa Benson (Benson's Rock Thrush) - inaainishwa pia kama nususpishi ya P. sharpei
- Monticola brevipes, Chatimwamba Madole-mafupi (Short-toed Rock Thrush)
- Monticola erythronotus, Chatimwamba wa Mlima Amber (Amber Mountain Rock Thrush) - inaainishwa pia kama nususpishi ya P. sharpei
- Monticola explorator, Chatimwamba Mlinzi (Sentinel Rock Thrush)
- Monticola imerina, Chatimwamba-pwani (Littoral Rock Thrush)
- Monticola rufocinereus, Chatimwamba Mdogo (Little Rock Thrush)
- Monticola rupestris, Chatimwamba Kusi (Cape Rock Thrush)
- Monticola saxatilis, Chatimwamba Mkia-mwekundu (Common au Rufous-tailed Rock Thrush)
- Monticola semirufus, Chatimwamba Mabawa-meupe (White-winged Cliff Chat)
- Monticola sharpei, Chatimwamba-misitu (Forest Rock Thrush)
- Monticola solitarius, Chatimwamba Buluu (Blue Rock Thrush)
Spishi ya Asia
[hariri | hariri chanzo]- Monticola cinclorhynchus (Blue-capped Rock Thrush)
- Monticola gularis (White-throated Rock Thrush)
- Monticola rufiventris (Chestnut-bellied Rock Thrush)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Chatimwamba-miyombo
-
Jike wa chatimwamba madole-mafupi
-
Chatimwamba wa Mlima Amber
-
Chatimwamba mlinzi
-
Chatimwamba-pwani
-
Chatimwamba mdogo
-
Chatimwamba kusi
-
Chatimwamba mkia-mwekundu
-
Chatimwamba mabawa-meupe
-
Chatimwamba-misitu
-
Chatimwamba buluu
-
Blue-capped rock thrush
-
White-throated rock thrush
-
Chestnut-bellied rock thrush