Nenda kwa yaliyomo

Poromoko la theluji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Banguko la theluji milimani.

Poromoko la theluji (pia banguko, kwa Kiingereza: avalanche[1]) ni kiasi kikubwa cha theluji au barafu kinachoanza kusogea kwenye mtelemko wa mlima na kuteleza au kuanguka kuelekea bondeni.

Mwendo wa masi kubwa unaweza kusukuma miamba, miti na chochote kilichopo njiani kwenye mtelemko wa mlima na kuongeza banguko.

Poromoko la theluji ni hatari kwa watu waliopo mlimani na pia kwa vijiji bondeni ambavyo vinafikiwa na banguko kubwa.

Katika Alpi za Ulaya takriban watu 100 hufariki kila mwaka kutokana na maporomoko ya theluji.

Kwenye Andes za Peru watu 4,000 waliuawa na poromoko kubwa la theluji tarehe 11 Januari 1962. Poromoko la theluji lilitelemka kutoka mlima Huascaran na kufunika mji wa Yungay; mengine yalianguka katika mto na kusababisha mafuriko.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Banguko si Kiswahili cha kawaida, ni msamiati wa KAST.