Popo-wadudu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Popo-wadudu
Popo pua-njumufarasi mdogo (Rhinolophus hipposideros)
Popo pua-njumufarasi mdogo
(Rhinolophus hipposideros)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda: Chiroptera (Wanyama kama popo)
Nusuoda: Microchiroptera (Popo-wadudu)
Dobson, 1875
Ngazi za chini

Familia 7 za juu:

Popo-wadudu ni aina za popo wanaowinda wadudu hasa. Kibiolojia ni mamalia wa nusuoda Microchiroptera katika oda Chiroptera wanaofanana na panya mwenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni ndogo kuliko zile za nusuoda Megachiroptera (popo-matunda) lakini kuna spishi zilizo kubwa kulika spishi fulani za popo-matunda. Spishi ndogo kabisa ni popo pua-nguruwe aliye na urefu wa mm 29-33 na uzito wa g 2. Kwa hivyo popo huyu ni spishi ndogo kabisa ya mamalia pia. Kirukanjia wa Etruski anaweza kuwa na uzito mdogo zaidi (g 1.2-2.7) lakini ni mrefu zaidi (mm 36-53). Popo-wadudu hula wadudu hasa lakini spishi nyingine hula samaki, ndege na wanyama wadogo na hata damu. Hutumia miwangwi ya sauti yao ili kuyakamata mawindo yao. Spishi kadhaa hula matunda na mbochi na hizi hazitumii miwangwi.

Uainisho (Simmons & Geisler, 1998[1])[hariri | hariri chanzo]

Oda: Chiroptera

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Simmons, N. B. and Geisler, J. H. (1998) Phylogenetic relationships of Icaronycteris, Archaeonycteris, Hassianycteris and Palaeochiropteryx to extant bat lineages, with comments on the evolution of echolocation and foraging strategies in Microchiroptera. Bulletin of the American Museum of Natural History, 235:1-182.