Popo-matunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Popo-matunda
Popo mwekundu (Rousettus aegyptiacus)
Popo mwekundu
(Rousettus aegyptiacus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda: Chiroptera (Popo)
Nusuoda: Megachiroptera (Popo-matunda)
Dobson, 1875
Familia: Pteropodidae
Gray, 1821
Ngazi za chini

Nusufamilia 7:

Popo-matunda ni aina za popo wanaokula matunda hasa. Kibiolojia ni mamalia wa familia Pteropodidae, familia pekee ya nusuoda Megachiroptera katika oda Chiroptera, wanaofanana na panya au mbwa mdogo mwenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni kubwa kuliko zile za nusuoda Microchiroptera (popo-wadudu) lakini kuna spishi zilizo ndogo kulika spishi fulani za popo-wadudu. Yumkini spishi kubwa kabisa ni popo-bweha wa Uhindi aliye na uzito wa kg 1.6, urefu wa mwili wa sm 40 na urefu wa mabawa wa hadi m 1.5. Mabawa ya popo-bweha mkubwa yana urefu wa hadi m 1.6. Spishi ndogo kabisa ni popo-matunda mabawa-madoa aliye na uzito wa g 15 na urefu wa mwili wa sm 5-6. Popo-matunda hula matunda au mbochi. Wale wanaokula matunda husambaza spishi za miti na wale wanaokula mbochi huchavusha maua. Kama popo wote hata popo-matunda hukiakia usiko na hulala mchana. Wakilala wananing'inia juu chini na kujifunika kwa mabawa. Takriban spishi zote hulala mitini, lakini spishi kadhaa hulala ndani ya mapango.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]