Nenda kwa yaliyomo

Pleteleti za damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pleteleti za damu; kushoto: hali ya kawaida; kulia: zikiwa tayari kuganda na kuziba pengo.
Picha ya hadubini elektronia ya ukaguzi (SEM) ya seli nyekundu ya kawaida ya damu, pleteleti ya damu, na seli nyeupe ya damu.

Pleteleti za damu au thrombositi (kutoka Kiingereza blood platelets, thrombocytes) pia seli sahani ni sehemu ya damu. Ni vipande vya seli visivyo na kiini. Zina umbo la kisahani chenye kipenyo cha µm 1.5 hadi µm 3.0.

Kazi yake ni kuziba vidonda vidogo. Kama seli za ndani ya mshipa wa damu zinavunjika, pleteleti zinakusanyika kwenye pengo hili na kushikamana pamoja yaani zinaganda na hivyo kuziba pengo. Kazi hii haiwezekani kama pengo ni kubwa mno. Ndiyo sababu ya kufunga kidonda kwa plasta au bendeji ili pleteleti ziweze kuziba pengo polepole.

Kama mtu ana idadi ndogo ya pleteleti kuna hatari ya kutokwa na damu kutokana na vidonda hasa ndani ya mwili visivyoonekana. Magonjwa kama malaria au homa ya dengi yanaweza kuathiri pleteleti.

Kama mtu ana kiwango kikubwa mno cha pleteleti za damu kuna hatari ya kuganda kwa damu kwenye mishipa na kuunda thrombasi, yaani kibonge cha pleteleti kinachozuia mwendo wa damu; hii ni hatari sana ikitokea ndani ya moyo au ubongo kwa kuwa inaweza kuleta kiharusi.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pleteleti za damu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.