Nenda kwa yaliyomo

Piet de Villiers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pieter Johannes de Villiers (19 Juni 1924 - 18 Mei 2015), alikuwa mpiga kinanda, na mtunzi wa nyimbo nchini Afrika Kusini. [1] Majina yake ya utani yalikuwa "Prof Piet" na "Piet Vingers". Anajulikana kwa kuunda mashairi ya Boerneef kwenye muziki, kufundisha piano na ogani, na kuwafundisha wanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini kwenye piano.

Alizaliwa huko Klerksdorp Magharibi mwa Transvaal Afrika Kusini . Alikuwa mtoto wa pili kati ya watoto watatu. Alikuwa na kaka mkubwa na dada mdogo. Wazazi wake walikuwa Leonard de Villiers na Johanna Christina du Toit. Baba yake Leonard alikuwa mwalimu mkuu wa shule na alicheza fidla(violin). [2]

Elimu na Taaluma

[hariri | hariri chanzo]

Pieter de Villiers alipata shahada ya kwanza mwaka wa 1942 katika Lugha za Kawaida katika Chuo Kikuu cha Pretoria . Mnamo 1946 alisoma chini ya Maprofesa Swanson, Fismer na Lubbe huko Stellenbosch . Alihitimu kama mwalimu wa muziki mnamo 1948. Mnamo 1954 aliteuliwa kama mhadhiri mdogo katika Chuo Kikuu cha Potchefstroom cha Elimu ya Juu ya Kikristo. Kuanzia mwaka wa 1962, alifundisha kinanda, na ogani katika Chuo Kikuu cha Pretoria . Pia alifanya kazi katika Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini kwa mwaka mmoja mnamo 1962. Alistaafu kutoka chuo kikuu mwaka wa 1985. [3] [4]

Alifariki akiwa nyumbani kwake Stellenbosch tarehe 18 Mei 2015.

  1. "Pieter Johannes de Villiers". Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Heunis, Daniela. "Two musical and political extremes in the South Africon society". heunis. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Well-known composer and pianist Pieter de Villiers dies at 90". de Villiers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-26. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Heunis, Daniela. "Two musical and political extremes in the South Africon society". heunis. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Heunis, Daniela. "Two musical and political extremes in the South Africon society". heunis
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Piet de Villiers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.