Paul Kipsiele Koech
Paul Kipsiele Koech (alizaliwa mnamo 1981 katika Cheplanget) ni mwanariadha wa Kenya katika mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji. Alishinda Nishani ya shaba katika mbio hizi katika mashindano ya Olimpiki ya 2004.
Maisha ya Utoto
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa mnamo 1981 katika sehemu ya Cheplanget, karibu na Mji wa Sotik, Wilaya ya Buret. Alifuzu kutoka Shule ya Sekondari ya Cheplanget mnamo 1999 Alitia fora katika Mbio za kitaifa za Masafa marefu na akaalikwa kukimbia Barani Uropa, akajiunga na Timu iliyokuwa ikisimamiwa na James Chepleton[1]. Licha ya kuwa mwanariadha wa kasi zaidi katika mbio hizo, Koech ameshindwa mara kadhaa katika majaribio ya kufuzu kwa Mashindano ya Dunia au Olimpiki kutoka Kenya. [2]. Alishiriki katika Finali za Dunia za All Seven zilizoandaliwa na IAAF.[3]. Pia alijenga Shule ya Msingi karibu na nyumbani kwake Yeye pia huwapa mafunzo ya Riadha Wanariadha chipukizi, akiwemo bingwa Chipukizi wa Dunia Mercy Cherono[4]. Koech ameoa na ana mtoto aliyezaliwa mnamo 2004.[1] na mdogo wa Kiume[2].
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Shindano | Mahali pa maandalizi | Matokeo | Habari ya Ziada |
---|---|---|---|---|
2003 | Michezo ya Bara Afrika | Abuja, Nigeria | nafasi ya 2 | |
Finali za IAAF | Monte Carlo, Monaco | nafasi ya 2 | ||
2004 | Michezo ya Olimpiki | Athens, Greece | nafasi ya 3 | Mita 3000 kuruka viunzi na maji |
Finali za IAAF | Monte Carlo, Monaco | nafasi ya 3 | ||
2005 | Ubingwa wa Dunia | Helsinki, Finland | 7th | Mita 3000 kuruka viunzi na maji |
finali za dunia za Riadha | Monte Carlo, Monaco | Mshindi | ||
2006 | Ubingwa wa bara Afrika | Bambous, Mauritius | mshindi | |
Finali za Dunia za Riadha | Stuttgart, Ujerumani | Mshindi | ||
Kombe la Dunia la IAAF | Athens, Greece | nafasi ya 2 | ||
2007 | Finali za Riadha za IAAF | Stuttgart, Ujerumani | Mshindi | |
2008 | Mashindano ya Ubingwa ya Ndani | Valencia, Spain | Nafasi ya 2 | mita 3000 |
Finali za riadha za IAAF | Stuttgart, Ujerumani | Mshindi | ||
2009 | Ubingwa wa Dunia | Berlin, Ujerumani | 4th | mita 3000 kuruka viunzi na maji |
Finali za Riadha za IAAF | Thessaloniki, Greece | Nafasi ya 2 | 3000 m kuruka viunzi na maji |
matokeo bora zaidi kwake
[hariri | hariri chanzo]- Shindano la mita 1500 - 3:37.92 (2007)
- Shindano la mita 3000 - 7:33.93 (2005)
- Maili mbili - 8:13.31 (2008)
- Shindano la mita 5000 - 13:11.26 (2005)
- Shindano la mita 3000kuruka viunzi na Maji - 7:56.37 (2005)
Tazama Pia
[hariri | hariri chanzo]Riadha Shirikisho la Riadha Duniani
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Paul Kipsiele Koech
- ↑ 1.0 1.1 21 Agosti 2004: Focus on Africa - Paul Kipsielei Koech (KEN) Ilihifadhiwa 1 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- ↑ 2.0 2.1 The Standard, 12 Agosti 2009: Kipsiele Ako na Matumaini ya Ushindi Berlin Ilihifadhiwa 13 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine.
- ↑ IAAF, 24 Septemba 2009: World Athletics Final û a statistical farewell
- ↑ x]
Sporting positions | ||
---|---|---|
Alitanguliwa na Saif Saaeed Shaheen |
Mita 3000 kuruka viunzi na Maji kwa wanaume, Matokeo bora zaidi ya Mwaka 2007 |
Akafuatiwa na Incumbent |
Makala hii kuhusu mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Makala hii inahusu wanariadha wa Olimpiki wa Afrika bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |