Paul Bomani
Paul Bomani | |
Paul Lazaro Bomani (1 Januari 1925 - 1 Aprili 2005) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania na balozi wa nchi hiyo huko Marekani na Mexico.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1960, Bomani alikuwa Waziri wa Maliasili na Maendeleo ya Ushirika katika serikali ya Tanganyika (1961-1964). Alishikilia nyadhifa nyingine kadhaa za uwaziri. Kati ya mwaka 1972 na mwaka 1983 alikuwa balozi wa Marekani na Mexico. Kuanzia mwaka 1992 hadi mauti ilipomkuta alikuwa mwenyekiti wa Tanzania Breweries Limited na Tanzania Distilleries Limited, kuanzia mwaka 1993 alikuwa kansela wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[1]
Bomani alipenda kujielezea kwa maneno yake mwenyewe hivi: Profesa wa Chuo alinielezea kama mbunifu mwenye busara, na kipawa cha kupanga na kuhamasisha watu. Nilikuwa mkono wa kulia wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru. Wasukuma walikuwa kabila kubwa zaidi nchini Tanganyika na walikua zaidi ya robo ya wakazi wa nchi hiyo wanaoishi katika ukanda wa Ziwa. Niliweza kusaidia machifu 50 wa jadi ya Kisukuma na kuwapa uaminifu na heshia kubwa. Kwa sababu ya mafanikio ya mashirika yetu ya kijamii na biashara ambayo ilikuwepo kabla ya kuundwa kwa TANU pia niliweza kupata heshima na imani kubwa kutoka kwa watu wa kisukuma, ambao walinipa jina la utani la "Kishamapanda" - maana yake ni "mtengeneza njia". Alifanya kazi zifuatazo: 1961 Waziri wa Maliasili na Maendeleo ya Ushirika.
- 1962 Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Tanganyika
- 1964 Waziri wa Fedha na Masuala ya Uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- 1965 Waziri wa Mambo ya uchumi na Mipango ya maendeleo
- 1970 Waziri wa Biashara, Viwanda na Madini
- 1972 -1983 Balozi wa Merika ya Amerika na Jamhuri ya Mexico
- 1983 Waziri wa Rasilimali na Madini
- 1984 Waziri wa Ardhi, Maliasili, Utalii na Nyumba
- 1986 Waziri wa Kilimo na Masoko
- 1988 Waziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii
- 1989 Waziri wa Serikali za Mitaa, Masoko, Ushirika na Maendeleo ya Jamii
- 1990 Ofisi ya Waziri wa Rais, inayohusika na Utekelezaji na Uratibu Sera ya Baraza la Mawaziri
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Late Ambassador Paul Bomani's Curriculum Vitae". Official Website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2007-08-02.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |