Panya-miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Panya-miti
Spishi fulani ya panya-miti (Graphiurus cf. murinus)
Spishi fulani ya panya-miti (Graphiurus cf. murinus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Sciuromorpha (Wanyama kama kindi)
Familia: Gliridae (Wanyama walio na mnasaba na panya-miti)
Muirhead, 1819
Jenasi: Chaetocauda Wang, 1985

Dryomys Thomas, 1906
Eliomys Wagner, 1840
Glirulus Thomas, 1906
Glis Brisson, 1762
Graphiurus Smuts, 1832
Muscardinus Kaup, 1829
Myomimus Ognev, 1924
Selevinia Belosludov & Bazhanov, 1939

Panya-miti ni wanyama wadogo wa familia Gliridae. Spishi nyingi hupanda miti na huishi katika matundu ya mti au tago la ndege. Wanyama hawa wanafanana na kindi mdogo. Urefu wa mwili wao ni kutoka mnamo sm 8 hadi sm 20 na wana mkia wenye urefu karibu na mwili. Rangi yao ni kahawia, kijivu au nyeusi na chini nyeupe kwa kawaida. Spishi nyingine zina mabaka. Hula beri, matunda na makokwa hasa lakini maua, majani, gamba la mti, wadudu na mayai pia. Jike huzaa hadi zaidi ya watoto 10.

Panya-miti wa kulika alikuwa huliwa sana na Warumi wa kale. Sikuhizi bado huliwa huko Slovenia

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Ulaya na Asia[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]