Mapafu
Mapafu ni sehemu ya mwili inayoingiza oksijeni mwilini na kuituma kwenye seli za mwili. Ni ogani kuu ya mfumo wa upumuaji, yaani tendo la kupumua.
Ni kawaida kwa wanyama wa faila ya chordata walio na uti wa mgongo na kupumua hewa.
Hutokea kwa jozi maana yake kuna mapafu mawili, si moja tu kama moyo.
Kuna pia samaki na konokono kadhaa wenye mapafu.
Mapafu huvuta hewa ndani ambamo oksijeni ya hewa inaingizwa katika damu na kupelekwa kwenda seli za mwili.
Ndani ya mapafu kuna viputo vidogo sana ambavyo ndio mwisho wa njia ya hewa kutoka nje. Damu inazunguka viputo hivi katika mishipa midogo inayotenganishwa na nafasi ya hewa kwa ngozi nyembamba sana. Oksijeni inaweza kupita kwenye ngozi na kuingia katika damu inapopokewa na seli za damu nyekundu.
Chordata walio wengi huwa na mapafu mawili.
Kuna wanyama wadogo wasio na mapafu. Wachache wanapokea oksijeni yote kupitia ngozi.
Njia nyingine ni wadudu walio na neli nyingi ndogo zinazoingiza hewa mwilini na kupokea oksijeni kupitia kuta za neli hizo.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- A revision site directed towards IGSCE students
- A to Z list of diseases of the Lung Ilihifadhiwa 18 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.
- List of Lung Cancer information sites Ilihifadhiwa 10 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- In depth articles on the lung
- In depth article on the anatomy of a lung
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mapafu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |