Nenda kwa yaliyomo

PBU

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Parliamentary Broadcasting Unit (kifupi PBU) ni mtandao wa televisheni za Kenya ambao uliundwa mwaka 2009 na Bunge la Kenya kwa msaada wa USAID kwa lengo la kupanua nafasi ya demokrasia[1]. Mtandao wa PBU hutangaza mijadala ya Bunge la Kenya.

Mtandao wa PBU una stesheni mbili za televisheni: Bunge TV, ambayo hutangaza vikao vya Bunge la Taifa la Kenya moja kwa moja, na Senate TV, ambayo hutangaza vikao vya Seneti ya Kenya moja kwa moja. Stesheni zote mbili zinapatikana kwenye Signet.