Nenda kwa yaliyomo

Mpunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Oryza)
Mpunga
(Oryza spp.)
Mpunga wa kiasia
Mpunga wa kiasia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Oryza
L.
Spishi: O. barthii A. Chev.

O. glaberrima Steud.
O. longistaminata Steud. & Roehr.
O. rufipogon Griff.
O. sativa L.
O. nivara S.D. Sharma & Shastry

Mpunga ni aina ya mimea katika familia ya manyasi (Poaceae). Spishi kadhaa zinapandwa katika sehemu mbalimbali za dunia, lakini mpunga wa kiasia ni ile ya kawaida.

Mpunga ni chanzo cha chakula kwa watu wengi duniani. Punje (mbegu) zake ni nafaka na huitwa mchele. Mchele uliopikwa ni wali.