Nenda kwa yaliyomo

Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Shughuli za Hisani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo la Ofisi ya OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Shughuli za Hisani (United Nations Office for the Coordination of Humanitarian Affairs OCHA) ni idara mojawapo kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Ofisi ya OCHA ina kazi ya kuratibu misaada ya kihisani pale ambapo majanga makubwa yanapita uwezo wa nchi au jumuiya fulani[1]. OCHA ilianzishwa mwaka 1991 kwa azimio la Mkutano Mkuu wa UM[2].

Inashiriki na taasisi nyingine za UM na nje za UM kama vile Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Msalaba Mwekundu, au WFP. Pamoja na kusaidia nchi mbalimbali kupambana na athira za Covid-19, OCHA ilihusika katika msaada kwa wakimbizi huko Afghanistan na Ethiopia na kusaidia nchi zilizopathiriwa na mafuriko au ukmame kama vile Bangladesh, Malawi na Somalia[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Our Work, tovuti ya OCHA, Desemba 2021
  2. History of OCHA, tovuti ya OCHA, Desemba 2021
  3. Our Work, tovuti ya OCHA, Desemba 2021