O.M.I.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya mwanzilishi, Mt. Eujeni Mazenod.

Missionary Oblates of Mary Immaculate (kifupi O.M.I.) ni shirika la kipapa la wamisionari lililoanzishwa na Eujeni Mazenod (1782-1861) tarehe 25 Januari 1816.

Mtakatifu huyo kutoka Ufaransa alipata kibali cha Papa Leo XII tarehe 17 Februari 1826.

Shirika linaundwa na mapadri na mabruda ambao kwa kawaida wanaishi kijumuia.

Mwaka 2011 walikuwa 4,400 hivi (kati yao 580 katika hatua za malezi) wakifanya umisionari katika sehemu nyingi za dunia, wakiwemo makardinali 2 na maaskofu wengi.[1]

Historia na karama[hariri | hariri chanzo]

Lengo la awali la shirika lilikuwa kuleta uamsho katika Kanisa Katoliki la Ufaransa baada ya Mapinduzi ya Kifaransa.

Lakini mapema kazi zake ziliongezeka na kuenea.[2] Papa Pius XI (1857-1939) alipendezwa na juhudi za wanashirika hata akawaita “Wataalamu wa misheni ngumu zaidi za Kanisa”[3]

Kama watawa wengine, wanashirika wanaweka nadhiri kuhusu mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu.

Wanashirika maarufu[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Generalate website: Who we are. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-02-23. Iliwekwa mnamo 2014-04-09.
  2. Australian Province: Oblate charism. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-06-01. Iliwekwa mnamo 2014-04-09.
  3. Philippine Province: Mission Today

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Carrière,, Gaston (1957), Histoire documentaire de la congrégation des Missionnaires Oblats de Marie-Immaculée dans l’Est du Canada. Vol. 1., Ottawa, Ontario: Éditions de l’Université d’Ottawa, 
  • Carrière,, Gaston (1957), Dictionnaire biographique des Oblats de Marie-Immaculée au Canada. Vol. 1-3., Ottawa, Ontario: Éditions de l’Université d’Ottawa, 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: