Nyota Ndogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nyota Ndogo (jina lake la kweli ni Mwanaisha Abdalla , na alizaliwa mwaka wa 1981 -tarehe kamili bado haijabainika) ni mwanamuziki kutoka Kenya ambaye huimba nyimbo za pop ambazo zimechanganywa na taarab.

Ndogo anatoka katika mji mkuu wa mwambao wa Mombasa. Alikuwa mwanafunzi wakati mmoja katika maisha yake lakini aliacha skuli kwa sababu zisizojulikana na baada ya kuacha skuli, alifanya kazi kama mjakazi wa nyumba. Babake, Atib Abdala , pia alikuwa mwanamuziki katika bendi ya mtaa, lakini Nyota Ndogo hakuchukua wasifu wa muziki hadi alipokuwa furahishwa sana na maneno katika muziki wa kundi la hip-hop la K-South. Baadaye, talanta yake iligunduliwa na Andrew Burchell, mtengeneza muziki mwenye makao katika mji mkuu wa Mombasa.

Nyota Ndogo ametoa Albamu tatu: Chereko , Nimetoka Mbali na Mpenzi .Alishinda tuzo la Kisima kwa kuwa mwimbaji bora muziki wa Taarab mwaka wa 2003 mwimbaji bora wa kike mwaka wa 2005. Alikuwa na teule tatu katika tuzo za Kisima za mwaka wa 2008. Aliteuliwa kwa tuzo la msanii bora wa kike wa kenya katika tuzo za PAM mwaka wa 2007. Wimbo wake wa Watu na Viatu uliteuliwa kama wimbo bora wa Afrika ya Mashariki mwaka wa 2007 katika tuzo za muziki za Tanzania.

Wimbo wake "Take Care" umeshirikishwa katika albamu ya mkusanyiko ya kimataifa ya World 2003 , huku wimbo wake wa "Chereko" ukiwa katika albamu ya mkusanyiko ya Rough Guide to the Music of Kenya na wimbo huo huo pia ulishirikishwa katika mkusanyiko wa Rough Guides - Off the Beaten Track .

Alishirikiana pamoja na mwanamuziki Nonini kwenye wimbo wa Nibebe na alishirikiana pia na kundi la Necessary Noize katika wimbo wa "Nataka Toa".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]