Nenda kwa yaliyomo

Norberto Murara Neto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Norberto Murara Neto

Norberto Murara Neto (anajulikana kama Neto; alizaliwa 19 Julai 1989) ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama kipa wa klabu ya Hispania Barcelona F.C..

Neto alianza kazi yake huko Brazili na klabu ya Athletico Paranaense na baadaye alihamia Fiorentina ya Italia. Mwaka 2015 alijiunga na Juventus , ambapo alishinda Seria A mara mbili, Yeye alikuwepo pale klabuni kama golikipa namba mbili ikiwa nyota Gianluigi Buffon ni golikipa namba moja, lakini alionekana kwenye michezo mingi ya Juventus ya ndani na nje ya Italia.

Mnamo mwaka 2017, alijiunga na Valencia ya Hispania. Mnamo 27 Juni, 2019 Barcelona ilitangaza kumsaini Neto.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Norberto Murara Neto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.