Njegere ya kizungu
Mandhari
Njegere za kizungu (jina la kisayansi kwa Kilatiniː Pisum sativum) ni mbegu za aina ya mimea ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali za dunia.
Mimea hii inapatikana katika spishi za Dicotyledonae katika himaya Plantae.
Mbegu za njegere za kizungu ni za mviringo kwa asili yake.
Njegere za kizungu zipo katika makundi mbalimbali kulingana na rangi za maua kama vile nyeupe, nyekundu na njano.
- Njegere huhitaji udongo wenye rutuba ili kustawi vizuri, pia huhitaji umwagiliaji wa mara kwa mara ndani ya wiki, walau mara mbili ndani ya wiki.
- Njegere hustawi zaidi sehemu zenye baridi na si zenye joto kali; kwa Tanzania hupatikana sehemu mbalimbali kama vileː Iringa, Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto) na Mbeya.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Njegere ya kizungu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |