Ni Wako

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Ni Wako"
Wimbo wa Makihiyo akiwa na Ben Pol
Umetolewa (audio 7 Disemba, 2017 - video 15 Disemba, 2017)
Umerekodiwa 2017
Aina ya wimbo Bongo Flava
Lugha Kiswahili
Urefu 3:30
Mtunzi Ben Pol
Mtayarishaji Tiddy Hotter

Ni Wako ni jina la wimbo ulioimbwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Norway, Makihiyo akimshirikisha Ben Pol kutoka Tanzania. Wimbo umetungwa na Ben Pol na kutayarishwa na Tiddy Hotter. Huu ni wimbo wa kwanza kutoa kwa msanii huyu chipukizi na amepanga kuimba mitindo mbalimbali ya muziki unaopatikana Tanzania.[1] Awali aliutambulisha kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 7 Disemba, 2017 na video yake kutoka tarehe 15 Disemba, 2017. Huku akiwa na ziara za kutembelea media mbalimbali kuanzia tarehe 12 Disemba 2017 hadi tarehe 2 Januari, 2018.[2] Wimbo unahusu wimbi zito la mahaba waliyonayo wapenzi wawili. Wanajibishana kwa ustadi wa hali ya juu kiasi kwamba sio rahisi kufahamu kama aliyeimba si Mswahili. Makihiyo kaonesha nia ya dhati ya kuimba na kupaisha muziki wa Bongo Flava anga nyingine.[3] Video ya wimbo huuu imeongozwa na Khalfani, ikionesha mazingira ya wakazi wengi wa Pwani, huko Bagamoyo. Lengo hasa ilikuwa kuleta umbo la asili la Mwafrika. Makihiyo anaonekana kushiriki katika michezo ya ngoma na vazi la khanga.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ni Wako "Makihiyo na Ben Pol sasa ‘Ni Wako’ " ingizo la tarehe 12-12-2017 - Bongo5.
  2. Makihiyo aliandika: "Ready for Tanzania Media Tour" katika ukurasa wake wa Instagram.
  3. Makihiyo ft. Ben Pol - Ni Wako (Official Audio) katika idhaa ya YouTube mnamo tarehe 7 Disemba, 2017.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Video ya Ni Wako katika YouTube