Naomba Kwako Bibiye
"Naomba Kwako Bibiye" | ||
---|---|---|
"Naomba Kwako Bibiye" kava | ||
Wimbo wa Ikhwani Safaa Musical Club
kutoka katika albamu ya A Hundred Years Of Taarab In Zanzibar | ||
Umetolewa | 1984/1985 | |
Aina ya wimbo | Taarab asilia | |
Urefu | 12:28 | |
Mtunzi | Maulid Machaprara | |
Mtayarishaji | Malindi | |
A Hundred Years Of Taarab In Zanzibar orodha ya nyimbo | ||
|
"Naomba Kwako Bibiye" ni jina la wimbo ulioimbwa na kundi zima la muziki wa taarab kutoka mjini Zanzibar, Ikhwani Safaa Musical Club au Malindi. Wimbo umetoka miaka ya 1980 na kuimbwa na marehemu Maulid Mohamed Machaprara. Wimbo unatoka katika albamu ya kompilesheni ya "A Hundred Years Of Taarab In Zanzibar". [1] Kompilesheni hii ilitazama nyimbo za Malindi tangu kuanzishwa kwake kuanzia 1905 hadi 2005. Wimbo huu ni wa 8 kutoka katika albamu hii. Machaprara anamlilia mpenzi wake anayejitia kisebusebu juu ya mapenzi yake kwake. Anambembeleza amtie mwake moyoni, kwani mengi ni mateso ashuhudiayo duniani hapa. Haishi hapo, ameonjeshwa raha ya mtu anayependwa, mbaya zaidi akamfanyia hila ya mapenzi.