Nabii Ahiya
Nabii Ahiya (kwa Kiebrania: אחיה השילוני, Aḥiyah[1] "YHWH ni ndugu yangu"[2]) alikuwa nabii wa kabila la Lawi kutoka Shilo wakati wa mfalme Solomoni, inavyoelezwa na Biblia ya Kiebrania (Kitabu cha kwanza cha Wafalme).
Ahiya ni maarufu hasa kwa kuwa alimtabiri Yeroboamu kwamba atakuwa mfalme wa makabila kumi wa Israeli Kaskazini (1Fal 11:29-39)[3].
Baadaye alimtabiria mke wa Yeroboamu I kifo cha mwanae na maangamizi ya ukoo wake pamoja na uhamisho wa Israeli hadi ng'ambo ya mto Eufrate (1Fal 14:6-16)[4].
Kadiri ya Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati, Ahiya alitunga pia kitabu chenye jina la "Unabii wa Ahiya wa Shilo" na taarifa kuhusu ufalme wa Solomoni (2Nya 9:29). Hata hivyo kitabu hicho hakijatufikia. Katika 1Fal 11:41 kinaitwa "Matendo ya Solomoni".
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ According to "Ahijah", Jewish Encyclopedia, the name also appears in the expanded form אחיהו, Aḥiyahu.
- ↑ See Gesenius, who interprets the name as "friend of Jehovah," taking the literal expression 'brother' as metaphorical for friendship. [1]
- ↑ "Ahijah", Jewish Encyclopedia
- ↑ Holman Bible Dictionary, "Beyond the River"
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nabii Ahiya kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |