My Way (albamu ya Usher)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
My Way
My Way Cover
Studio album ya Usher
Imetolewa 1997
Aina R&B
Urefu 40:21
Lebo LaFace/Arista Records
Mtayarishaji Jermaine Dupri
Wendo wa albamu za Usher
Usher
(1994)
My Way
(1997)
Live
(1999)
Single za kutoka katika albamu ya My Way
  1. "You Make Me Wanna..."
    Imetolewa: 1997
  2. "Nice and Slow"
    Imetolewa: 1997
  3. "My Way"
    Imetolewa: 1998
  4. "Bedtime"
    Imetolewa: 1998

My Way ni jina la kutaja albamu ya pili ya mwimbaji-mtunzi wa R&B Usher. Albamu ilitolewa ba studio ya LaFace Records mnamo tar. 16 Septemba ya mwak wa 1997. Single maarufu kutoka kwenye albamu hii, ni pamoja na "You Make Me Wanna", "My Way", na "Nice and Slow".

Pia inajumlisha ule wimbo alioimba na msanii wa kike maarufu kwa jina la Monica, na wimbo uliitwa Slow Jam, ukiwa kama kibwagizo cha filamu ya Soul Food, ambao awali uliimbwa na kundi la muziki la zamani la Midnight Star mnamo mwaka wa 1983.

Kwa bahati, ameanza zaidi ya kopi milioni sita kwa U.S. na zaidi ya milioni nane kwa hesabu ya dunia nzima na kuifanya kuwa albamu yake ilivyovunja rekodi ya albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina lake mwenyewe iliyopata mauzo hafifu.

Hii ni albamu ya Usher iliyofupi zaidi, yaani albamu ina nyimbo kumi tu. Albamu imepata kushika nafasi ya 4 katika U.S., nafasi ya 3 katika Kanada na 16 katika UK. Single zote zilizotoka kwenye albamu hii zimepata mafanikio makubwa kabisa, zikiwa single zote zimeshika nafasi ya kwanza au ya pili kwa U.S. na You Make Me Wanna ikashika nafasi ya kwanza katika UK na kuufanya wimbo wa kwanza wa Usher kushika nafasi ya kwanza katika UK.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

  1. "You Make Me Wanna..." - 3:39
  2. "Just Like Me" (akimshirikisha Lil' Kim) - 3:26
  3. "Nice & Slow" - 3:48
  4. "Slow Jam" (akimshirikisha Monica) - 4:40
  5. "My Way" - 3:38
  6. "Come Back" - 3:47
  7. "I Will" - 3:55
  8. "Bedtime" - 4:45
  9. "One Day You'll Be Mine" - 3:24
  10. "You Make Me Wanna..." (Toleo Lililoongezwa) - 5:20

Sampuli[hariri | hariri chanzo]

One Day You'll Be Mine

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]