Mwelekeo mkuu wa dira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dira inayoonyesha mielekeo mikuu.

Mwelekeo mkuu wa dira (kwa Kiingereza: cardinal direction au cardinal point) ni nukta nne zinazoonekana kwenye dira: Kaskazini, Mashariki, Kusini na Magharibi.

Ufafanuzi wa mielekeo mikuu[hariri | hariri chanzo]

Kaskazini na Kusini ni mielekeo ambayo hulenga ncha za kijiografia upande wa kusini na kaskazini wa Dunia. Mzunguko wa Dunia kwenye mhimili wake unafafanua Mashariki na Magharibi. Jua linachomoza kila asubuhi mashariki na kutua magharibi. Ncha za kijiografia za kaskazini na kusini ziko karibu na ncha sumaku za Dunia.

Kama sindano ina tabia ya sumaku na kuruhusiwa mwendo bila kuzuiwa (kwa mfano ikielea juu ya uso wa maji) itajipanga kulingana na uga sumaku wa Dunia kwa hiyo kujipanga kwa kuelekeza ncha zake kwenda ncha sumaku yaani kaskazini na kusini.

Kwenye dira sindano sumaku inaweza kucheza kwenye mhimili wake.

Tofauti baina ncha jiografia na ncha ya dira[hariri | hariri chanzo]

Ilhali ncha sumaku kwa kawaida si sawa kamili na ncha za kijiografia kuna tofauti ndogo baina ya kaskazini ya dira na kaskazini ya kijiografia. Tofauti si muhimu sana katika maeneo yaliyo karibu na ikweta, huwa kubwa zaidi kadiri dira inavyotumiwa karibu zaidi na ncha za Dunia.

Mielekeo mikuu katika Kiswahili cha mabaharia[hariri | hariri chanzo]

Kiswahili cha mabaharia kilikuwa na maneno mengine kama vile:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. α Alpha Carinae
 2. E. Steere, A handbook of the Swahili language as spoken at Zanzibar, London 18752, p. 365
 3. Steere, p. 294: Kibula, the kebla, the point to which men turn when they pray. Among the Mohammedans the kibula is the direction in which Mecca lies, which is in Zanzibar nearly north. Hence kibula is some times used to mean the north.
 4. Steere p. 361
 5. Sacleux, Charles. 1939. Dictionnaire Swahili - Français. (Travaux et Mémoires de l'Institut d'Ethnologie, Vols. 36/37), uk. 501, ila kwa kawaida kwa kutaja nchi za Waarabu zilizopo upande wa kaskazini wa Uswahilini
 6. A.C. Madan, English-Swahili Dictionary, Oxford 1903, p. 112 online hapa; kwa "mao" angalia Krapf, A dictionary of the Suahili language, London 1882, online hapa, 201
 7. Krapf 190
 8. Sacleux uk. 485 anaandika "maČèo", kwa lahaja za kusini OS. Ngw. = DN. malwèo,ma!èo
 9. Madan, p. 453
 10. Krapf uk. 201
 11. Krapf uk. 411 alisikia lugha ya "mfuma nguo" kwa mashariki na "mfuma ngozi" kwa magharibi "The sun rises in the East among those people who make, wear and sell clothes, whereas the sun sets in the West with those people who make skins, which they wear."