Mwanamke wa kijijini na ajira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mwanamke wa kijijini anapatikana katika jamii inayoishi vijijini, wengi wao wanajihusisha na shughuli za kilimo, ufugaji na ujasiriamali; wanafanya kazi kwa nguvu lakini kipato chao ni kidogo. [1]

Wanawake wa namna hiyo hukumbana na vitendo mbalimbali vya kikatili kwa sababu pengine hawaruhusiwi kumiliki ardhi kama wanaume, wengi wao hufanyiwa vitendo hivyo na waume zao pamoja na watu wengine ndani ya familia zao japokuwa wanaleta mchango mkubwa wa kiuchumi katika familia na jamii kwa ujumla.

Vikwazo vya kiuchumi[hariri | hariri chanzo]

Wanawake wa vijijini hukumbana na vikwazo mbalimbali katika kuboresha maisha yao kiuchumi na kijamii; vizuizi hivyo huhusisha ukosefu wa mikopo, ukosefu wa huduma za afya na elimu na wakati mwingine hupata ujuzi kidogo. Changamoto hizo hujumuisha pia mshahara mdogo katika ajira.[2][3]

Jitihada za kumuendeleza mwanamke kijijini[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya kazi za wanawake ambazo hazina malipo, tafiti mbalimbali zinaendelea ili kutengeneza sera na mipango kwa ajili ya wanawake wa vijijini.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kak, Shakti (1994). "Rural Women and Labour Force Participation". Social Scientist 22 (3/4): 35–59. ISSN 0970-0293. JSTOR 3517622. doi:10.2307/3517622. 
  2. Gender, Equality and Diversity & ILOAIDS Branch (2018-03-06). "Rural Women at Work: Bridging the gaps". www.ilo.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-08. 
  3. "The role of women in rural development, food production and poverty eradication". UN Women – Headquarters (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-08. 
  4. Koolwal, Gayatri B. (2021-11-01). "Improving the measurement of rural women's employment: Global momentum and survey priorities". World Development (kwa Kiingereza) 147: 105627. ISSN 0305-750X. doi:10.1016/j.worlddev.2021.105627 – kutoka World Bank Group. 
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanamke wa kijijini na ajira kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.