Kwaya
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mwanakwaya)
Kwaya (kutoka Kiingereza "choir" au "quire") ni kundi la waimbaji au uimbaji wa watu kwa pamoja.
Kuna aina mbalimbali za kwaya lakini hapa tunaorodhesha baadhi tu ya aina hizo.
- Kwaya ya wanawake: Hii ni kwaya inayojumuisha wanawake (watu wa jinsia ya kike) pekee bila wanaume (watu wa jinsia ya kiume). Kwaya ya namna hii kwa kawaida huwa na sauti mbili tu, yaani sauti ya kwanza (Soprano) na sauti ya pili (Alto).
- Kwaya ya watoto: Hii ni kwaya inayoundwa na watoto tu. Kwaya hii nayo kwa kawaida huwa na sauti mbili kama ilivyo kwaya ya wanawake pekee.
- Kwaya ya wanaume: Aina hii ya kwaya hujumuisha wanaume pekee. Hii pia huwa na sauti moja hadi mbili kwa kawaida, lakini wakati mwingine huwa hata na sauti zote nne. Hii sasa si kwa kwaya ya wanaume tu bali hata kwaya ya wanawake pia hata ya watoto kufuatia maendeleo ya kimuziki wataalamu wameendelea kugundua uwezekano wa kutengeneza sauti zote nne kama ilivyo katika kwaya ya mchanganyiko.
- Kwaya ya mchanganyiko: Hii hujumuisha wote, wanaume na wanawake hata na watoto pia. Kama yalivyo maelezo ya hapo juu; aina hii ya kwaya kwa kawaida huwa na sauti zote nne yaani yaani sauti ya kwanza (Soprano), sauti ya pili (Alto), sauti ya tatu (Tenor) na sauti ya nne (Bass).
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kwaya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |