Mustapha Anane
Mustapha Anane (Larbaâ Nath Irathen, 1950 - 21 Oktoba 2010) alikuwa mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Algeria ambaye alitumia maisha yake yote katika klabu ya JS Kabylie. [1]
Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Anane alizaliwa katika mji wa Larbaâ Nath Irathen na kukulia katika wilaya ya Lalla Saïda huko Tizi Ouzou, ambapo alianza kucheza kandanda katika mtaa wake. [2]
Ushiriki Katika Klabu
[hariri | hariri chanzo]Akiwa na umri wa miaka 14, Anane alijiunga na safu ya chini katika klabu ya JS Kabylie. Miaka minne baadaye, kocha wa timu ya wakubwa, Ali Ben Fedda, alimpandisha kwenye kikosi ambapo alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Dinamo Minsk ya Umoja wa Kisovyeti.
Ushiriki Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Licha ya kuwa mchezaji wa kawaida wa Timu ya Taifa ya Algeria, Anane aliichezea timu hiyo mara mbili pekee, akicheza mechi za kirafiki dhidi ya Hungary na Albania.
Kazi ya usimamizi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya maisha yake ya uchezaji, Anane alifundisha timu za chini na za wakubwa katika klabu ya ndani ya AS Tizi Ouzou, pamoja na vilabu vingine katika eneo la Kabylie kama vile Les Issers, na mahali alipozaliwa, Larbaâ Nath Irathen.
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 21 Oktoba 2010, Anane alifariki mapema asubuhi huko Tizi Ouzou. [3] ambapo Alizikwa siku iyo hiyo katika Makaburi ya M'douha mjini humo.
Heshima
[hariri | hariri chanzo]- Alishinda kombe la ligi Algeria Championnat National mara nne akiwa na klabu ya JS Kabylie mnamo 1973, 1974, 1977, 1980.
- Alishinda Kombe la Algeria mara moja akiwa na JS Kabylie mnamo 1977
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ APS (Oktoba 21, 2010). "L'ancien joueur de la JS Kabylie, Mustapha Anane s'éteint à l'age de 60 ans". El Watan. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-10-23. Iliwekwa mnamo 2010-10-21.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Reportage – Mustapha Annane Archived 2010-11-19 at the Wayback Machine
- ↑ "Mustapha Anane n'est plus". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-26. Iliwekwa mnamo 2010-10-22.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mustapha Anane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |