Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Muddyb/Archive 4

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.

Asante

Asante kwa mapongezi yako ya tarehe 19 mwezi uliopita. Nami nakutakia kila la kheri kwa Mwaka Mpya. Wako katika kukuza lugha ya taifa, Baba Tabita (majadiliano) 15:04, 7 Januari 2009 (UTC)

Nawe pia--Mwanaharakati (Longa) 15:59, 7 Januari 2009 (UTC)

Hi Muddyb, could translate en:Gianluca Ramazzotti in Swahili? I thank you in advance!

Hi Muddyb, is ok? I write you if please you could translate in swahili the article on my friend Gianluca, in change I will translate in Sicilian dialect Dar es Salaam. Is it all right? In attends him I thank as always you in advance!--Lodewijk Vadacchino (majadiliano) 13:25, 8 Januari 2009 (UTC)

Currently, I'm not sure if I'll be able to write it righ away. If you give me sometime, I will definetely write it for you! You have my words. --Mwanaharakati (Longa) 13:40, 8 Januari 2009 (UTC)

Imefanyika..--Mwanaharakati (Longa) 07:58, 24 Januari 2009 (UTC)

Jamii za kata

Salaam, Muddy nimeanzisha jamii:kata za mkoa wa mbeya lakini naona heri nisiendelee. Naomba tuelewane. Kata zote inaweza kujaza mno jamii ya mkoa. Lakini kwa upande mwingine - nadhani afadhai kuziweka moja kwa moja kwenye jamii:wilaya ya XYZ. Afadhali kuliko kuzificha mno. Kwenye ngazi ya wilaya ita kuwa ni sawa. Unaonaje? --Kipala (majadiliano) 12:04, 10 Januari 2009 (UTC)

Aha, kwa hiyo kila wilaya iwe na JAMII ya kata zake, si ndiyvyo? Maana yake kata zote awali nilikuwa nikiziweka kwenye mkoa wake. Kwa mfano: Kata ya Kiwalani, Tabata, Mwenge, n.k... Nimeziweka zote kwenye JAMII ya Dar es Salaam kwa mujibu wa maelezo yako ya awali. Ama unataka vipi hapo?--Mwanaharakati (Longa) 13:18, 10 Januari 2009 (UTC)
Niseme kweli sina uhakika. Wewe unaonaje: majina haya yote katika jamii moja ni sawa au la? Yaani ukurasa moja ya jamii inaweza kushika majina 70-100 nisipokosei. Kama 80 ni kata hakuna kingine sawa. Lakini kama makala mengine yanaingia - tungehitaji ukurasa wa pili. Hapa naona heri kuwa na jamii za chini. KAma ni nyingi hivi afadhali kuzipanga kwenye wilaya (moja kwa moja, si kama kata ya wilaya). Unaonaje? --Kipala (majadiliano) 17:15, 10 Januari 2009 (UTC)
Eti umeona Kikunde‎? Mtumiaji asiyeandikishwa aliongeza habari ! Hii ilikuwa tumaini langu ya kwamba mtu fulani ataona jina la mahali anakotoka kumbe atavutwa kuongeza habari za mahali. Hakujua namna ya kufanya kwa hiyo ilinibidi nisahihishe kidogo. Lakini nafurahi - tuone ni wangapi watakaofuata. Asante kwa kuanzisha idara hii, mwenzangu! --Kipala (majadiliano) 02:25, 12 Januari 2009 (UTC)
Salaaam! Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu, kwani huku kwetu kulikuwa na Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar! Hivyo sikuweza kuja kazini kwa siku ya Jumatatu na Jumapili kama ilivyoada! Haya, hongereza zote zirudi kwako kwa kutoa wazo la kuanzisha makala hizi, kwani mie mwenyewe sikuwa na wazo la karibu kufikia kuandika makala za miji ya kwetu! Hivyo hongera nawe! KUHUSU KATA NA JAMII: Naunga mkono hoja la kuweka JAMII husika katika kila Wilaya kuliko zote kuziweka kwenye JAMII ya mkoa wake. Hivyo kutoka sasa tutahitajika kuumba JAMII kwa kila mkoa tutakao amia! Lakini hapa bado nina sawali moja: JAMII za chini zitaitwaje? Yaani endapo tutaanzisha JAMII:KATA ZA WILAYA YA MBOZI - kwa mfano, jamii ya chini itakuwa ipi?--Mwanaharakati (Longa) 06:15, 13 Januari 2009 (UTC)

Majina ya kata

Napendekeza kutofautisha majina ya kata kadhaa tangu mwanzo. Mfano majina kama Masoko, Majengo, Uzunguni, Mabatini n.k. ni kawaida mahali pengi. Naona afadhali tukifikiri ni jina linalotumiwa penginepo tuongeze jina la wilaya katika mabano.

Mzee wangu, ukiona mahali panajhitaji sahihisho we fanya tu, kwani mie kuhusu miji sina kawaida ya kuindika! Hivyo sina uzoefu wa kutunga makala nzuri za miji! Kazi njema--Mwanaharakati (Longa) 09:37, 13 Januari 2009 (UTC)

Bot

I can definately request it there, but according to what I read at Wikipedia:Jumuia this wiki follows Automatic approval which requires me to do 100 test edits and then request a steward at meta to grant me the flag. -Djsasso (majadiliano) 12:42, 14 Januari 2009 (UTC)

Ok I will post my request there. Thanks! -Djsasso (majadiliano) 13:04, 14 Januari 2009 (UTC)

Kata

Muddy, salamu naona unachapa kazi tena. Sasa nimetambua kitu kimoja: Ukishughulika makala za Lindi kumbe wilaya ziko tayari isipokuwa bila "Wilaya ya"... nadhani Oliver aliziweka kitambo. Sehemu ziko pia na majina ya kata. Mfano: Orodha ya Liwali ina "Liwali (mji)" na wewe ulianzisha sasa hivi "Liwale Mjini". Labda kabla ya kuanzisha kigezo uchungulie kama wilaya na majina ya kata zipo tayari. Mimi nimeweka orodha ya kata amoja na kiungo katika wilaya kadhaa. HApa nimeongeza mara moja jina la wilaya kwa mabano; kwa hiyo ukianzisha mbegu za kata hizi vema kuona orodha kwanza ili tusipate kata kwa maumbo mawili tofauti. Pia mimi napendekeza kuweka jina öla wilaya kwa mabano kama jina la kata ni kawaida yaani kama uwezekano upo lipo mahali pengine pia (kama: mamba,mnara, majengo n.k.) --Kipala (majadiliano) 09:45, 17 Januari 2009 (UTC)

Sijambo, Kipala. Ni kweli. Lakini safari hii sijakulupuka kama nilivyofanya awali kwenye Wilaya moja hivi. Na pia, bado ninafuata ule utaratibu uliousema wa kutumia jina la kata (kwa wilaya yake) na sio "kata." Ninashukuru kwa ushauri wako na bado nitaendelea kuusikiliza na kuufuata ushauri wako! Kila la kheri!--Mwanaharakati (Longa) 09:54, 17 Januari 2009 (UTC)
Bwana Muddy habari za asubuhi. Unaendelea kuchapa wilaya na kata. Naona mawili: Kwanza tuweke kigezo cha kata pia ukurasa wa wilaya (mimi nilianza kwa kuweka orodha ya kata ndani ya makala lakini vigezo vyako afadhali). Halafu tutumie geo-stub pia kwa makala za wilaya badala ya "mbegu" pekee. Ni hayo tu. Sijui unatumia mbinu gani kutengeneza vigezo? Mimi ninanakili jedwali la sensa kutoka intaneti, kupitia editor, halafu excel inapotokea tena kama jedwali na baadaye ni kazi dogo kunakili nguzo ya majina tu. Ukitumia MS-Word tena ni rahisi kubadilisha alama ya line-break kuwa mabano ya mraba mara moja kwa majina yote. Hapa kuna pia nafasi kuiambia Excel kupanga majina kufuatana na abc (mimi napendelea kama ni kazi ndogo). --Kipala (majadiliano) 07:39, 22 Januari 2009 (UTC)
Za asubuhi nzuri mzee wangu! Ninashukuru kwa ushauri wako wa kuweka geo-stub kwenye kila makala ya Wilaya. Pia, ninashukuru tena kwa kunipa ushauri wa kutumia Excel na MS-Words kwa kunakilia zile. Huruma ni kwamba sijawhi kunakili zile jedwali kwa kutumia hizo prog. Mara nyingi huwa natumia njia ya kunakili yale kutoka kwenye tovuti husika halafu nayapeleka kule kwenye wikipedia yakiwa vilevile (kwa lengo la kuyaweka kule yanajipanga kwa mfululizo ulele wa tovuti) - kisha ninayanakili kutoka wiki kwenda kwenye WORDPAD.EXE huku wordpad hiyo ikiwa na vibox vitupu vya kuweka viungo na maelezo mengine yaliyomo muda wote! Ni njia ndefu, lakini ninaifanya kwa sekunde chache sana. Na ndiyomaana nikiandika kata hizi nachukua mda mchache tu, nishamaliza kata 20 au 30!--Mwanaharakati (Longa) 08:03, 22 Januari 2009 (UTC)
Kingine: Maelezo yote nishaandika kila kitu kwa mfano, Wilaya na Mkowa wake, jamii, na vigezo vyote. Ninachofanya pale ni kubadilisha idadi ya watu tu. Ninakili kutoka internet halafu na paste kwenye wordpad. Ikiwa inahifadhi ukurasa, mie huku ninanakili tena na tena.... Usijali. It's an African mbinu. --Mwanaharakati (Longa) 08:11, 22 Januari 2009 (UTC)
HAya naona una pia mbinu wako. Kwa kunakili kutoka ukurasa wa intaneti mimi napitia kwenye programu ya "editor" inayopatikana kati ya "Start- All programs - accessoires". (katika nakala kadhaa za windows jina ni tofauti, alama yake ni ile kadaftari buluu). Faida yake ni inaondoa alama zote za html zinazokuja nikobandika kopi ya inteneti kwenye word. Kunakili jedwali naanza juu hadi chini ya jedwali. Halafu kutoka editor naipeleka kwenye excel ili niwe na nguzo tena na hivyo napata majina yote pekee. Orodha hii napanga a-b-c kwa "data-sort". Sasa nairudisha kwenye editor na kutoka hapa kuja Word(ili kuondoa alama za jedwali ifike Word kama maandishi matupu lakini unaweza kuiweka pia katika word na kubadilisha fomatu ya table kuwa text). Na katika Word naona nguzo ile ya majina na hapa natumia edit-replace; mwisho wa kila mstari kuna alama ya "line break" isiyoonekana kwa kawaida lakini kodi yake ni "^p", ukisema badilisha "^p" kuwa "]]^p[[" tayari umeshapata kila jina kwa mabano yetu ya wikipedia. Baadaye kwa matumizi ya orodha kwenye kigezo unaibadilisha "^p" kuwa " | " na tayari jinsi unavyoitaka kwa kigezo. Mara umeizoea inaenda chapchap.--Kipala (majadiliano) 12:24, 22 Januari 2009 (UTC)
Sawa. Lakini mimi mara nyingi huwa na highlight kile kijedwali cha hesabu ya watu halafu ninakipaste kwenye wikipedia. Sasa bado nina swali moja: Wewe una nakili vipi?--Mwanaharakati (Longa) 13:37, 22 Januari 2009 (UTC)

Labda uangalie picha:

Faili:Kunakili picha.JPG

Halafu hiyo unayoisema ni "NOTEPAD?"--Mwanaharakati (Longa) 13:43, 22 Januari 2009 (UTC)

Ninanakili jinsi unavyoonyesha. (Mimi: kwa kutumia panja, halafu rightclick-copy (au badala ya kopi kwa panya: ctrl-c). Lakini sasa una kopi ya jewali lote.
  1. njia rahisi kupata nguzo (column) ya majina tu ni kuipeleka katika excel. Kabla ya kuipeleka Excel nataka kuondoa alama za html zilizofichwa (kwa sababu zinakwamisha haraka kumbukumbu ya kompyuta na kuchelewesha kazi).
  2. Kwa hiyo naitupa kwanza mahali pasipopokea html. Mfano ni ile notepad/editor (iko kwa majina mawili kwenye kila mashine ya windows: start-programs-accessoires-); njia nyingine ni kuitupa katika ukurasa wa kuhariri wa wikipedia; kutoka hapa naikata (mark-rightclick) na kuipeleka kwenye ukurasa tupu wa excel. Kwenye excel (au programu nyingine ya aina hii) inajipanga tena kwa nguzo, nafuta nguzo za namba nabaki na majina ya kata tu.
  3. Hizi nakata tena na kuipeleka word - afadhali kupitia notepad (editor) tena inayoondoa alama za siri za excel
  4. katika word naweza kuongeza mara moja alama za ]] na [[. Hapa ni vema kujua amri zinazohusu alama zisizoonekana. Kama majina yapo kama nguzo katika word (kila kata msatri mmoja) natumia Find/Replace: find: ^p na replace ]]^p[[. Tayari orodha ya kata zenye mabano yetu. Kwa kigezo hatua inayofuata: Find ]]^p[[ replace ]] | [[. Jaribu!
    (ANGALIZI: nimeona ya kwamba kwa sababu zisizoeleweka jedwali kadhaa za sensa hazinakiliwi kama jedwali - utaiona mara moja katika editor - kama ni hivi - basi!--Kipala (majadiliano) 20:26, 25 Januari 2009 (UTC)
Muddy salaam nimekamilishia vigezo vya mikoa ya Morogoro na Iringa pamoja na Mtwara vijijini. Viko kwenye kuraza za wilaya. Ukipenda chukua kwa kata! --Kipala (majadiliano) 20:08, 25 Januari 2009 (UTC)
Kipala, sijambo. Kuhusu kunakili: Hapa naona shida moja ya kuziweka hizo kata kwa mfumo wa alfabeti oda. Mara nyingi zitapalaganyika kiasi iwe tabu katika kutafuta kata, kuliko ukiziacha kama zilivyo yaani utaanza moja kisha mbili kama jinsi ilivyo kwenye mfululizo wake wa tovuti ya taifa. Kingine: Hizo kata zote nitaziadika wala usihofu, ila kwa sasa kidoogo siko sawa. Nimebanwa kinamna fulani, lakini ninaahidi kutekeleza kazi hiyo! Ubarikiwe. --Mwanaharakati (Longa) 11:47, 26 Januari 2009 (UTC)
Kupata abc-oda nachezea tena kati ya word na excel nikipitia kwenye editor. Lakini naona sasa unaweza kuisort pia katika word. Sharti majina yote yawe kwa umbo kama nguzo (kila jina mstari mpya) halafu unamark yote, unapiga menu "table" halafu "sort" tayari abc. Baadaye unafanya kama juu Na. 4 kwa kutumia find/replace. --Kipala (majadiliano) 17:17, 26 Januari 2009 (UTC)

Salaam naona unachapa kazi kweli Mbeya iliyokuwa nyumbani kwangu. Asante. Nimekamilisha vigezo vya wilaya za Mara na Manyara. Kilimanjaro haina vigezo bado lakini kuna orodha ya kata kwenye makala ya kila wilaya. --Kipala (majadiliano) 21:37, 29 Januari 2009 (UTC)

Salam nawe! Ni kweli. Ninafuata agizo lako la kuendeleza vile vigezo vyote ulivyoviumba vya kata na wilaya za Tanzania! Basi nawe usisite kuongezea vitu kwenye kata hizo za Mbeya kwa awali ulishaishi kule! Naona bado nipo Mbeya, lakini nikitoka hapa nitaelekea kule Morogoro, ambako awali nilisema nitafanya! Salam nyingi kutoka Dar es Salaam, Tanzania zikufikie huko Ujerumani uliko. Ni mimi kijana wako,--Mwanaharakati (Longa) 06:55, 30 Januari 2009 (UTC)

Muddyb attention they want to cancel the article! Think of us you I pray you!--Lodewijk Vadacchino (majadiliano) 23:02, 25 Januari 2009 (UTC)

Dear Friend, apologizes if I have been an idiot with you. But I have been badly when they have cancelled the article of Lola and I have had to take absolute rest. However I don't forget the friends, especially a polite friend as you! Tomorrow I finish translating Dar es Salaam in Sicilian. Still excuse me Dear Friend! I hope that you won't have become angry or disappointed of me. Thanks still for the courtesy that shows. W Tanzania W Father Apollinaris!--Lodewijk Vadacchino (majadiliano) 23:51, 31 Januari 2009 (UTC)

Hello, Lodewijk Vadacchino. I didn't get angry for what you've done to me. I was just trying to remind you about the words you gave me! That is why I came over your Wiki to remind you, though. Your welcome, friend. Cheers,--Mwanaharakati (Longa) 06:26, 2 Februari 2009 (UTC)