Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Lucas559/Anorexia nervosa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lucas559/Anorexia nervosa
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuTaaluma ya tiba ya magonjwa ya akili
DaliliUzani mdogo, hofu ya kuongeza uzani, hamu kubwa ya kutaka kuwa mwembamba, kujizuia kula chakulas[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeMiaka ya ujana hadi miaka ya mapema ya utu uzima[1]
VisababishiHavijulikani[2]
Sababu za hatariHistoria ya familia, michezo ya riadha ya ngazi za juu, uanamitindo, kucheza densi[2][3][4]
Utambuzi tofautiUgonjwa wa dysmorphic wa mwili, bulimia nervosa, ugonjwa wa kutumia dawa za kulevya, hyperthyroidism, ugonjwa wa kuvimba matumbo, dysphagia, saratani[5][6]
MatibabuTiba ya Utambuzi wa Tabia, kulazwa hospitalini ili kurejesha uzani[1][7]
Utabiri wa kutokea kwakeHatari ya kufa ya asilimia 5% katika kipindi cha miaka 10[3][8]
Idadi ya utokeaji wakeWatu milioni 2.9 (mwaka wa 2015)[9]
Vifo600 (mwaka wa 2015)[10]

Anoreksia nervosa, ambao mara nyingi hujulikana kama anoreksia,[11] ni ugonjwa wa kula, unaojulikana kwa dalili za mtu kuwa na uzani mdogo, kujizuia kula chakula, hofu ya kuongeza uzani na hamu kubwa ya kutaka kuwa mwembamba.[1] Watu wengi walio na ugonjwa wa anoreksia hujiona kuwa wanene kupita kiasi ingawa kiukweli wana uzani mdogo.[1][2][12] Mara nyingi wao hukataa kuwa wana shida ya kuwa na uzani mdogo.[3][13] Wanajipima uzani mara kwa mara, hula kiasi kidogo ha chakula na hula vyakula fulani pekee.[1] Watu wengine hufanya mazoezi kupita kiasi, hujilazimisha kutapika au kutumia dawa za kupunguza uzani.[1] Matatizo yake yanaweza kujumuisha ugonjwa wa mifupa kuwa laini (osteoporosis), utasa na uharibifu wa moyo, miongoni mwa mengine.[1][14] Wanawake mara nyingi huacha kupata hedhi.[3]

Kisababishi chake hakijajulikani kwa sasa.[2][15] Inaonekana kwamba kuna baadhi ya vipengele vya kijenetiki ambapo mapacha wanaofanana huathirika mara nyingi zaidi kuliko mapacha wasiofanana.[2] Mambo ya kitamaduni pia yanaonekana kuwa na athari kwani jamii zinazothamini watu wembamba kuwa na viwango vya juu vya ugonjwa huu.[3] Isitoshe, ugonjwa huu hutokea kwa kawaida zaidi miongoni mwa watu wanaohusika katika shughuli zinazothamini wembamba kama vile michezo ya riadha ya ngazi za juu, uanamitindo na uchezaji densi.[3][4] Ugonjwa wa anoreksia mara nyingi huanza kufuatia kutokea kwa tukio linaloleta mabadiliko makubwa katika maisha au kusababisha mfadhaiko.[3] Utambuzi wake unahitaji mtu kuwa uzani mdogo sana.[3] Ukali wa ugonjwa huo hutegemea uwiano wa uzani wa mwili na kimo (BMI) kwa watu wazima walio na ugonjwa huu mdogo huwa na BMI inayozidi 17, BMI ya wastani ya 16 hadi 17, BMI mbaya ya 15 hadi 16 na BMI mbaya sana ya chini ya 15.[3] Kwa watoto BMI kulingana na asilimia ya umri ya chini ya asilimia 5 hutumiwa mara nyingi.[3][16]

Matibabu ya anoreksia yanahusisha kurejesha uzani mzuri kiafya, kutibu matatizo ya kisaikolojia yaliyopo na kushughulikia tabia zinazokuza tatizo hili.[1][17] Ingawa dawa hazisaidii katika kuongeza uzani, zinaweza kutumika kusaidia kudhibiti hali ya wasiwasi au mfadhaiko unaohusiana na ugonjwa huu.[1] Aina kadhaa za tiba zinaweza kuwa muhimu, kama vile tiba ya utambuzi wa tabia au mbinu ambapo wazazi huchukua jukumu la kulisha mtoto wao inayojulikana kama tiba ya familia ya Maudsley.[1][18] Wakati mwingine watu wanahitaji kulazwa hospitalini ili kurejesha uzani. Ushahidi wa manufaa yanayotokana na ulishaji kupitia mirija ya nasogastriki, hata hivyo hauko wazi.[19] Baadhi ya watu walio na anoreksia huwa na kipindi kimoja tu kisha wanapona huku wengine wanaweza kuwa na vipindi vingi kwa muda wa miaka mingi. Matatizo mengi huboreka au kutatuliwa kadri unapoonggeza uzani.

Kote ulimwenguni, ugonjwa wa anoreksia unakadiriwa kuathiri watu milioni 2.9 kufikia mwaka wa 2015.[9] Ugonjwa huu unakadiriwa kutokea kwa kati ya asilimia 0.9% hadi 4.3% ya wanawake na asilimia 0.2% hadi 0.3% ya wanaume katika nchi za Magharibi katika kipindi fulani cha maisha yao.[20] Takriban asilimia 0.4% ya wanawake vijana huathirika katika mwaka fulani na inakadiriwa kutokea mara kumi zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.[3] [20] Viwango vyake katika nchi nyingi zinazoendelea havijulikani.[3] Mara nyingi huanza katika umri wa miaka ya ujana au mwanzoni mwa utu uzima.[1] Ingawa ugonjwa wa anoreksia uligunduliwa zaidi katika karne ya 20, haijulikani ikiwa hili lilitokana na kuongezeka kwa idadi ya kutokea kwake au ilikuwa ni kwa sababu ya utambuzi bora zaidi.[2] Katika waka wa 2013 ugonjwa huu ulisababisha vifo vya moja kwa moja vipatavyo 600 ulimwenguni, kutoka vifo 400 vya mwaka wa 1990.[21] Ugonjwa wa kula pia huongeza hatari ya mtu kukufa kutokana na visababishi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujiua.[1][20] Takriban asilimia 5% ya watu walio na ugonjwa wa anoreksia hufa kutokana na matatizo yaliyotokea katika kipindi cha miaka kumi, hatari iliyoongezeka karibia mara sita.[3] Neno "anorexia nervosa" lilitumiwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1873 na William Gull kuelezea hali hii.[22]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 "What are Eating Disorders?". NIMH. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Attia E (2010). "Anorexia nervosa: current status and future directions". Annual Review of Medicine. 61 (1): 425–35. doi:10.1146/annurev.med.050208.200745. PMID 19719398.
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (tol. la 5). Washington: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 338–345. ISBN 978-0-89042-555-8.
  4. 4.0 4.1 Arcelus J, Witcomb GL, Mitchell A (Machi 2014). "Prevalence of eating disorders amongst dancers: a systemic review and meta-analysis". European Eating Disorders Review. 22 (2): 92–101. doi:10.1002/erv.2271. PMID 24277724.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Parker, Robert; Sharma, Asheesh (2008). General Medicine (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 56. ISBN 978-0723434610. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2020.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. M.D, Michael B. First (19 Novemba 2013). DSM-5 Handbook of Differential Diagnosis. American Psychiatric Pub. ISBN 9781585624621. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2020 – kutoka Google Books.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Feeding and eating disorders" (PDF). American Psychiatric Publishing. 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 1 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 9 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Espie J, Eisler I (2015). "Focus on anorexia nervosa: modern psychological treatment and guidelines for the adolescent patient". Adolescent Health, Medicine and Therapeutics. 6: 9–16. doi:10.2147/AHMT.S70300. PMC 4316908. PMID 25678834.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  9. 9.0 9.1 Vos, Theo; Allen, Christine; Arora, Megha; Barber, Ryan M.; Bhutta, Zulfiqar A.; Brown, Alexandria; Carter, Austin; Casey, Daniel C.; Charlson, Fiona J. (Oktoba 2016). "Global, regional, and national incidence, prevalence, and years lived with disability for 310 diseases and injuries, 1990-2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1545–1602. doi:10.1016/S0140-6736(16)31678-6. PMC 5055577. PMID 27733282.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Wang H, Naghavi M, Allen C, Barber RM, Bhutta ZA, Carter A, na wenz. (GBD 2015 Mortality and Causes of Death Collaborators) (Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980-2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/S0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Sari Fine Shepphird (2009). 100 Questions & Answers About Anorexia Nervosa. Jones & Bartlett Learning. uk. xvi. ISBN 978-1-4496-3079-9. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Attia E (2010). "Anorexia nervosa: current status and future directions". Annual Review of Medicine. 61 (1): 425–35. doi:10.1146/annurev.med.050208.200745. PMID 19719398.
  13. Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (tol. la 5). Washington: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 338–345. ISBN 978-0-89042-555-8.
  14. "What are Eating Disorders?". NIMH. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. Attia E (2010). "Anorexia nervosa: current status and future directions". Annual Review of Medicine. 61 (1): 425–35. doi:10.1146/annurev.med.050208.200745. PMID 19719398.
  16. Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (tol. la 5). Washington: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 338–345. ISBN 978-0-89042-555-8.
  17. "What are Eating Disorders?". NIMH. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. Hay P (Julai 2013). "A systematic review of evidence for psychological treatments in eating disorders: 2005-2012". The International Journal of Eating Disorders. 46 (5): 462–9. doi:10.1002/eat.22103. PMID 23658093.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. "Eating Disorders: Core Interventions in the Treatment and Management of Anorexia Nervosa, Bulimia Nervosa and Related Eating Disorders.". 
  20. 20.0 20.1 20.2 Smink FR, van Hoeken D, Hoek HW (Agosti 2012). "Epidemiology of eating disorders: incidence, prevalence and mortality rates". Current Psychiatry Reports. 14 (4): 406–14. doi:10.1007/s11920-012-0282-y. PMC 3409365. PMID 22644309.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. Naghavi M, Wang H, Lozano R, Davis A, Liang X, Zhou M, na wenz. (Januari 2015). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385 (9963): 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMC 4340604. PMID 25530442.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. Gull WW (Septemba 1997). "Anorexia nervosa (apepsia hysterica, anorexia hysterica). 1868". Obesity Research. 5 (5): 498–502. doi:10.1002/j.1550-8528.1997.tb00677.x. PMID 9385628.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)