Mtolondo-kanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtolondo-kanga
Mtolondo-kanga koo-pinki
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Amadina Swainson, 1827

Clytospiza Shelley, 1896
Emblema Gould, 1842
Euschistospiza Wolters, 1943
Hypargos Reichenbach, 1862
Mandingoa Salvadori, 1884
Stagonopleura Reichenbach, 1850
Taeniopygia Reichenbach, 1862

Spishi: Angalia katiba

Mitolondo-kanga ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mitolondo lakini ndege hawa wana madoa meupe mengi tumboni. Wana rangi mbalimbali kama nyekundu, machungwa, kijani, kahawia, kijivu na nyeusi. Hula mbegu hasa na beri na wadudu pia. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 4-6.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]