Mto Marne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marne
{{{maelezo_ya_picha}}}
Chanzo Grand Est
Mdomo Seine
48°48′57″N 2°24′40″E / 48.81583°N 2.41111°E / 48.81583; 2.41111 (Seine-Marne)Coordinates: 48°48′57″N 2°24′40″E / 48.81583°N 2.41111°E / 48.81583; 2.41111 (Seine-Marne)
Urefu 514 km

Marne ni mto wa Ufaransa, tawimto upande wa kulia wa Seine katika eneo la mashariki na kusini ya Paris. Una urefu wa 514 kilometres (319 mi).[1] Mto ulizipatia jina lake wilaya za Haute-Marne, Marne, Seine-et-Marne, na Val-de-Marne.

Kisiwa katika mto Marne karibu na Chelles

Mto Marne unaanza katika platuu ya Langres, unatiririka kuelekea kaskazini, kisha unaelekea magharibi kati ya Saint-Dizier na Châlons-en-Champagne, na kuungana na Seine katika Charenton katika Paris. Katika kanda la Champagne sehemu ya maji huongozwa katika ziwa la kujengwa na binadamu la Lac du Der-Chantecoq, ili kudhibiti mtiririko wa maji. Kwa njia hiyo kiwango cha maji cha chini huzuiwa.[2]

Mto Marne ulikuwa eneo la mapigano mawili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. La kwanza Lilikuwa mgeuko wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika mwaka wa 1914. La pili lilitokea miaka minne baadaye, katika mwaka wa 1918.

Katika karne ya 19 na 20, Marne ulipendeza wachoraji na wasanii wengi; miongoni mwao ni:

Wilaya na miji iliyopitwa na mto huu[hariri | hariri chanzo]

Ufuko wa Marne katika Noisy-le-Grand


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Marne at the Sandre database (French).
  2. Apprivoiser la Marne (French). Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-11-24. Iliwekwa mnamo 2006-06-02.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Marne kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.