Msikiti Mkuu wa Djenné
Mandhari
Msikiti Mkuu wa Djenné ni jengo kubwa la matofali au adobe katika mtindo wa usanifu wa Sudano-Sahelian. Msikiti huu uko katika mji wa Djenné, Mali, kwenye uwanda wa mafuriko wa Mto Bani.
Msikiti wa kwanza kwenye eneo hilo ulijengwa karibu na karne ya 13, lakini muundo wa sasa ulijengwa mwaka 1907.
Mbali na kuwa kitovu cha jamii ya Djenné, ni moja ya alama maarufu zaidi barani Afrika. Pamoja na "Miji ya Kale ya Djenné", uliteuliwa na UNESCO kuwa kituo cha Urithi wa Dunia mwaka 1988.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |