Mshale wa Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Arrow of God  
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:

Arrow of God ni riwaya ya 1964 ya Chinua Achebe. Ni riwaya ya tatu Achebe ikifuata Things Fall Apart na No Longer at Ease. Vitabu hivi vitatu wakati mwingine huitwa The African Trilogy(utatu wa Afrika). Riwaya hii inahusu Ezeulu, kuhani mkuu wa vijiji kadhaa vya Nigeria, ambaye anatishana na nguvu za kikoloni na wamisionari wa kikristo katika miaka ya 1920. [1]

Utangulizi wa Vitimbi[hariri | hariri chanzo]

Kitabu hiki kimeandikwa katika mazingira ya vijiji vya Waigbo wa Nigeria. Ezeulu ni kuhani mkuu wa mungu Ulu, anayeabudiwa na vijiji sita vya Umuaro. Kitabu hiki kinaanza na Ezeulu na Umuaro kuanza vita na kijiji jirani cha Okperi. Mgogoro huu unatatuliwa mara moja wakati TK Winterbottom, mwangalizi wa kikoloni wa Uingereza anapoingilia.

Baada ya vita, mmisionari Mkristo, Yohana Goodcountry, anafika Umuaro. Goodcountry anawasimulia wanavijiji hadithi za Wanigeria katika Niger Delta ambao wameacha (na kuzipinga) "mila zao mbaya," na kupendelea Ukristo. Kwa kuamsha ghadhabu za jamii yake ya kitamduni, Ezeulu anamtuma mwanawe kujifunza kwa Goodcountry.

Ezeulu anaitwa mbali na kijiji chake na Winterbottom, na anaalikwa kuwa sehemu ya utawala wa ukoloni, sera inayojulikana kama kiwakala. Ezeulu anakataa kuwa "chifu wa mzungu" na anatupwa gerezani. Katika kijiji cha Ezeulu, watu hawawezi kuvuna vikuu kabla hajaidhinisha, lakini, kwa hasira ya kuwa gerezani, anakataa. Vikuu vinaanza kuoza mashambani na kupelekea njaa. Riwaya huitwa "Arrow of God" kwa sababu Ezeulu hujilinganisha na mshale katika upinde wa mungu. Anadai kuwa matatizo ambayo ameyaleta kijijini ni mapenzi ya Ulu. [2]

Wengi wa wanakijiji tayari wamepoteza imani yao katika Ezeulu. Mwana mwingine wa Ezeulu anaaga dunia katika sherehe za kitamaduni, na wanakijiji wanatafsiri hii kama ishara kwamba Ulu amemwacha kuhani wao. Badala ya kukabiliana na njaa tena, wanakijiji wanageuka na kuwa Ukristo.

Mandhari[hariri | hariri chanzo]

Ulu, vijiji vya Umuaro na Okperi, na maafisa wa kikoloni wote ni tamthilia. Lakini Nigeria katika miaka ya 1920 ilikuwa ikitawaliwa na mamlaka ya kikoloni ya Uingereza, kiwakala ilijaribiwa kama mkakati wa serikali, na wengi wa Waigbo kuacha imani yao ya jadi kwa Ukristo. Riwaya hii inachukuliwa kama kazi ya fasihi ya Afrika (mtindo wa realism).

Riwaya ya kwanza ya Achebe Things Fall Apart inazungumzia hadithi ya Okonkwo, kiongozi katika jamii yake hadi ukoloni unapoingia. Arrow of God vile vile inaelezea kuanguka kwa kiongozi wa kitamaduni katika mikono ya ukoloni. Migogoro mikuu ya riwaya hii inahusu mapambano kati ya mwendelezo na mabadiliko, kama vile Ezeulu kukataa kumtumikia Winterbottom, au kati ya wanakijiji wa jadi na mwana wa Ezeulu ambaye anasoma Ukristo. [2]

Vifananishi[hariri | hariri chanzo]

Neno "Arrow of God" limetolewa kutoka mithali ya Igbo ambapo mtu, au wakati mwingine tukio, husemekana kuwakilisha mapenzi ya Mungu. [3]. Arrow of God pia inajihusisha kimsingi na Traditional Acquiescence of Traditional African forms kwa ushawishi wa Ulaya.

Kutambuliwa[hariri | hariri chanzo]

Arrow of God ilishinda tuzo la kwanza kuwahi kuweko la Jock Campbell / New Statesman kwa uandishi wa Afrika. [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Arrow of God na Chinua Achebe", Time Magazine. Retrieved on 2007-09-19. Archived from the original on 2012-10-20. 
  2. 2.0 2.1 Mathuray, Mark (2003). "Realizing the Sacred: Power and Meaning in Chinua Achebe's Arrow of God". Research in African Literatures 34 (3): 46. 
  3. Smith, Daniel Jordan (22 Septemba 2001). "'The arrow of God' pentecostalism, inequality, and the supernatural in South-Eastern Nigeria.". Africa 71 (4): 587. ISSN 0001-9720. doi:10.2307/1161581.  Check date values in: |date= (help)
  4. [8] ^ Ezenwa-Ohaeto Chinua Achebe: wasifu __: James Currey Ltd ISBN 0852555458 ukurasa 105

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]