Nenda kwa yaliyomo

Hakuna Starehe Tena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
No Longer at Ease  
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:

No Longer at Ease ni riwaya ya mwaka wa 1960 iliyoandikwa na mwandishi wa Nigeria Chinua Achebe.

Ni hadithi ya mtu Muigbo (pia huandikwa Muibo), Obi Okonkwo, ambaye anatoka kijijini mwake kutafuta elimu ya Uingereza na ajira katika utumishi wa kikoloni wa Nigeria, lakini anapambana kubadili hadi maisha ya Ulaya na kuishia kuchukua hongo. Kitabu hiki ni mwema kwa Things Fall Apart, cha Chinua Achebe ambacho kinahusu mapambano ya babu yake Obi Okonkwo dhidi ya mabadiliko yaliyoletwa na Waingereza.

Kichwa cha riwaya hii[hariri | hariri chanzo]

Kichwa cha kitabu hiki kinatokana na mistari ya mwisho ya shairi lake TS Eliot, The journey of the Magi(= "safari ya mamajusi"):

We returned to our places, these Kingdoms,(Tulirudi kwenye maeneo yetu, hizi falme,
But no longer at ease here, in the old dispensation,(Lakini hakuna starehe tena, katika mapumziko ya uzeeni,
With an alien people clutching their gods.(Kukiwa na watu wageni walionata na miungu yao).
I should be glad of another death.(lazima nitafurahi nikifa.)

Muhtasari wa Vitimbi[hariri | hariri chanzo]

Riwaya inaanza na kesi ya Obi Okonkwo akistakiwa na madai ya kupokea hongo. Halafu inaturudisha nyuma hadi wakati kabla yake kuelekea Uingereza na inaendelea kuelezea vile Obi alijipata kotini.

Wanachama wa Shirikisho la Maendeleo ya Umuofia (UPU), kundi la wanaume Waigbo waliokuwa wametoka vijijini mwao na kuenda kuishi katika miji mikuu ya Nigeria, wamefanya mkusanyiko wa kumtuma Obi Uingereza kusoma sheria, kwa matumaini kwamba angerudi kuwasaidia watu wake kukabili jamii ya ukoloni ya Uingereza. Lakini Obi anapofika huko, anageuza hadi somo la Kiingereza.

Obi anarudi Nigeria baada ya miaka minne ya masomo na anaishi mjini Lagos na rafiki yake Joseph. Anapata kazi katika Bodi ya Udhamini na mara moja anapewa hongo na mtu ambaye anajaribu kupata udhamini wa dada yake mdogo. Wakati Obi anakataa kwa hasira kuchukua hongo, msichana mwenyewe anamtembelea ambaye anaashiria kutaka kumhonga kwa ngono ili apate udhamini, ahadi ambayo Obi anakataa.

Wakati huo huo, Obi anaendeleza uhusiano wa kimapenzi na Clara, msichana Munigeria ambaye hatimaye anafichua kwamba yeye ni osu, aliyelaaniwa na ukoo wake, maana yake ikiwa kwamba Obi hawezi kumuoa kwa njia ya kitamaduni ya Waigbo wa Nigeria. Wakati anabaki dhamira kumuoa Clara, hata baba yake ambaye ni Mkristo anapinga, na mama yake anamsihi huku akiwa katika kitanda chake cha kifo kuwa asimuoe Clara mpaka baada ya kifo chake, huku akitishia kujiua ikiwa Obi hangetii. Wakati Obi anampasha Clara matukio haya, Clara anajitoa kwenye mahusiano na anatangaza kwamba yeye ni mjamzito. Obi anapanga kutoa mimba, jambo ambalo Clara analifanya shingo upande, lakini anapata matatizo na anakataa kumuona Obi baadaye.

Wakati huu wote, Obi anajipata katika matatizo ya kifedha, moja kwa sababu ya kutokua na mipango, pili kwa sababu ya haja ya kulipa mkopo wake kwa UPU na kuwalipia watoto wao elimu na tatu kwa sababu ya gharama utoaji mimba usio halali.

Anapopata habari za kifo cha mama yake , Obi anapatwa na unyogovu, na anakataa kwenda nyumbani kwa mazishi. Wakati anapopona, anaanza kupokea rushwa huku akisita kukiri kwamba ni njia ya ulimwengu wake.

Riwaya inaisha wakati Obi anachukua hongo na anajiambia kuwa ni ya mwisho anapokea, bila yeye kujua kwanga hongo hii ndiyo ingemletea balaa. Anakamatwa, tukio ambalo linatuleta mwanzoni mwa hadithi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]