Monte Rosa
Mandhari
Monte Rosa ni safu ya milima ya Alpi kati ya nchi za Italia na Uswisi (Ulaya).
Urefu wa kilele chake kirefu kabisa huitwa Dufourspitze na ni mita 4,634 juu ya usawa wa bahari, hivyo ni wa pili kati ya milima yote ya Ulaya Magharibi. Vilele vingine ni Dunantspitze (mita 4,632), Grenzgipfel (mita 4,618) na Nordend (mita 4,609).