Monie Love

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Monie Love
Jina la kuzaliwa Simone Gooden
Pia anajulikana kama Monie Love
Amezaliwa 2 Julai 1970 (1970-07-02) (umri 53)
Asili yake London, England
Aina ya muziki Hip hop
BritHop
New jack swing
Kazi yake Rapa, mwimbaji wa hip hop
Miaka ya kazi 1989–hadi sasa
Studio Warner Bros. Records
Cooltempo/Chrysalis/EMI Records
Tuff Groove
Ame/Wameshirikiana na Native Tongues
Dave Angel

Simone Gooden (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Monie Love; amezaliwa 2 Julai 1970) ni emcee kutoka nchini Uingereza na mtangazaji wa redio wa zamani huko nchini Marekani.

Alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika hip hop ya Kiingereza, na kuleta mgongano/athira kubwa na wasaili/maemcee wengine wa kike wa Kimarekani kama vile Queen Latifah, vilevile kupitia uanchama wake na baadhi ya makundi mwishoni mwa miaka ya 1980/mwanzoni mwa miaka ya 1990 - Native Tongues. Love alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza wa BritHop kuingia mkataba na kusambaziwa kazi zake dunia nzima na mastudio makubwakubwa duniani.

Miaka ya awali[hariri | hariri chanzo]

Love alizaliwa katika eneo la Battersea la mjini London. Huyu ni mdogo wake mwnamuziki wa muziki wa techno Dave Angel, na alikuwa binti wa baba aliyekuwa akipiga muziki wa jazz kutoka mjini London.

Shughuli za muziki[hariri | hariri chanzo]

Love alizanza kazi yake ya hip hop/BritHop akiwa kama emcee kwenye kundi la Kiingereza la Jus Bad, kundi ambalo linaunganishwa na DJ Pogo, Sparki, na MC Mell'O'. Kundi hilo lilitoa kibao cha kilichokwenda kwa jina la "Free Style/Proud" katika studio moja ya kujitegemea Tuff Groove mnamo 1988.

Love alianza kujipatia umaarufu wake wa kujulikana kibiashara nchini Marekani baada ya kuuza sura katika single ya Queen Latifah iliyojishindia Grammy Award "Ladies First," vilevile kwenye kibao cha Adeva "Ring My Bell," na kwa kina Jungle Brothers' "Doin' Our Own Dang," na kibao kikali cha kina De La Soul "Buddy." Umaarufu huo umepelekea kuingia mkataba na Warner Bros. Records, inamfanya Love kuwa miongoni mwa wasanii wachacha sana wa British hip-hop kufanya juhudi za kutoa kazi zao na mastudio makubwakubwa duniani.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu zake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Nafasi ya chati
U.S. U.S. R&B
1990 Down to Earth 109 26
1993 In a Word or 2 75

EP/Single alizofanya akiwa kivyake[hariri | hariri chanzo]

Maelezo ya Albamu
Slice Of Da Pie EP

Single Alizoshirikishwa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Monie Love