Moise Kean
Moise Bioty Kean (matamshi ya Kiitalia: [mɔize kɛn]; alizaliwa 28 Februari 2000) ni mchezaji wa soka wa Italia ambaye anacheza kama winga wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Vercelli na wazazi wa Ivory Coast. Kean mara ya kwanza alionwa na ndugu yake Renato Biasi akicheza mpira, ambaye alimshauri acheze timu za vijana wa Asti,Alimsikiliza na kufuata mashauri yake, akaonesha kiwango kizuri na akachukuliwa na klabu ya Torino mwaka 2013.
Mnamo 19 Novemba 2016, akiwa na umri wa miaka 16, aliingia uwanjani dakika ya 84 baada ya kutolewa Mario Mandžukić kwa kushinda 3-0 dhidi ya Pescara, na hivyo akawa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa katika miaka ya 2000 kushindana katika mojawapo ya ligi nne za Ulaya . Mnamo 22 Novemba 2016, akawa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa katika miaka ya 2000 kucheza mechi za Mabingwa wa Ulaya UEFA.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Moise Kean kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |