Mohammed Maulid Ali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mohammed Maulid Ali ni mwanasiasa, mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Alichaguliwa kuwa mbunge wa kata ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja nchini Tanzania kwa miaka 20202025. [1] Mnamo mwaka 1975 mpaka 1979 alifanya kazi kama mhasibu msaidizi katika taasisi ya Kibo Paper Industries ya Dar es salaam na ilipofika mwaka 1980 mpaka 2016 alifanya kazi kama mwongoza meli za kigeni katika Shirika la Meli la Zanzibar.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]