Nenda kwa yaliyomo

Mohamed Elneny

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elneny akiwa Arsenal.
Elneny akiwa Arsenal.

Mohamed Naser Elsayed Elneny (anajulikana kama Mohamed Elneny; alizaliwa 11 Julai 1992) ni mchezaji wa soka wa Misri ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Uingereza Arsenal FC na timu ya taifa ya Misri.

Alianza kazi yake katika timu ya Al Ahly ya Misri, alihamia klabu ya Uswisi FC Basel mwezi Januari 2013. Alishinda ligi mara nane huko Basel, ikiwa ni pamoja na Swiss Super League.

Mnamo Januari 2016 alihamia Arsenal, uhamisho wake ulithibitishwa rasmi na klabu kuwa kati ya £ milioni 5 na £ milioni 7.4. Alipewa jezi namba 35 mgongoni.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohamed Elneny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.