Mocco Genius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mocco Genius
Amezaliwa Oktoba 4 1993 (1993-10-04) (umri 30)
Asili yake Lindi Tanzania
Kazi yake Mtayarishaji
Miaka ya kazi 2017 - Mpaka sasa
Studio Imagination Sound
Tovuti https://moccogenius.wordpress.com/

Idd Mohamed Ngomba (anajulikana kama Mocco Genius) alizaliwa tarehe 04 Oktoba 1993 huko Lindi katika pwani ya kusini mashariki mwa Tanzania. Hivi sasa yuko Dar Es Salaam, Tanzania. Kwa sasa ni mtayarishaji wa nyimbo kutoka Tanzania. Anajulikana zaidi kwa kutayarisha nyimbo maarufu za Bongo Fleva kama "Cheche" ya Zuchu akimsirikisha Diamond Platnumz, "Omukwano" ya Tommy Flavour akimshirikisha Alikiba, Pia amehusika kutayarisha wimbo wa "Inatosha" wa Mwanamuziki maarufu Marioo na nyingine nyingi.

Kama mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Imagination Sound, studio ya kurekodi muziki jijini Dar es Salaam, Tanzania ambayo ni maarufu kwa kutengeneza vibao vya Bongo Flava, Mocco ana mchango mkubwa katika tasnia ya muziki ya Afrika Mashariki.

Mocco amefanya kazi na wanamuziki mashuhuri kutoka kote barani Afrika na ameweza kutengeneza nyimbo na wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Mbosso, Zuchu, Marioo n.k..[onesha uthibitisho]


References[hariri | hariri chanzo]

MOCCO GENIUS : ALI KIBA ALIWAAMBIA WACHAGUE/ MBOSSO MSHIKAJI WANGU SANA .........

BIRTHDAY PARTY YA MOCCO GENIUS YAWAKUTANISHA USO kwa USO MAPRODUCER TZ NAKUTENGENEZA BEAT ya PAMOJA

Meet Mocco Genius: The Man behind Top Hits in Tanzania

Mocco Genius Lyrics, Songs, and Albums | Genius

Latest Mocco Genius Songs 2021 | Mocco Genius MP3 Music Archived 28 Aprili 2021 at the Wayback Machine.

Mocco Genius Aibukia kwenye Bongo Fleva