Mkutano wa YouLead

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkutano wa YouLead Arusha 2020.

YouLead Summit ni mkutano wa vijana viongozi kutoka Afrika ya Mashariki unaofanyika kila mwaka mwezi wa Novemba kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya uongozi na changamoto zinazoyakabili mataifa na vijana katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Mkutano huu huwakutanisha vijana kutoka nchi za Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda na Sudani Kusini [1]

Mwaka 2020 mkutano wa Youlead ulifunguliwa na rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ukiwa na kauli mbiu ya Maendeleo ni Watu (Development is People), na kwa mara ya kwanza mkutano huu ulifanyika kwa njia ya Video na watu kuweza kuufuatilia kupitia mitandao ya kijamii [2] Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu imechukuliwa kutoka katika nukuu za Mwalimu Nyerere ,Maendeleo ni Watu. [3]

Youlead 2019[hariri | hariri chanzo]

Mkutano wa YouLead Mwaka 2019 uliwakutanisha jumla wa vijana 325 ukiwa na kauli mbiu Leaving no one Behind pamoja na malengo ya umoja wa Afrika (Agenda 2063). [4]

Katika maandalizi ya mkutano huu, watu hutuma maombi ya kushiriki kwa njia ya mtandaona mkutano huu hutayarishwa na kituo cha MS-TCDC kilichopo Arusha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-24. Iliwekwa mnamo 2020-11-24. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-24. Iliwekwa mnamo 2020-11-24. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-06. Iliwekwa mnamo 2020-11-25. 
  4. http://www.cac.ac.tz/blog/2019/8/9/120-hungry-visitors-ndwsp-5tccd-kat5m