Nenda kwa yaliyomo

Mizari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mizari
(Dzeta Ursae Majoris, Mizar)[1]
Mizari (chini) inaonekana kama nyota maradufu kwa darubini ya wastani; juu iko Alcor
Kundinyota Dubu Mkubwa (Ursa Major)
Mwangaza unaonekana 2.27
Idadi kufuatana na Hummel, C. A (1998)
Kundi la spektra A2 V
Paralaksi (mas) 38.01 ± 1.71
Umbali (miakanuru) 86
Masi M☉ 2.43
Nusukipenyo R☉ 2.4
Mng’aro L☉ 33.2
Jotoridi usoni wa nyota (K) 9000
Majina mbadala Mizat, Mirza, Mitsar, 79 Ursae Majoris, BD+55 1598A, CCDM J13240+5456AB, FK5 497, GC 18133, HD 116656, HIP 65378, HR 5054, PPM 34007, SAO 28737


Mizari (lat. & ing. Mizar pia ζ Dzeta Ursae Majoris, kifupi Dzeta UMa, ζ UMa) ni kati ya nyota angavu katika kundinyota ya Dubu Mkubwa (Ursa Major). Ina umaarufu kama nyota maradufu inayoonekana kwa macho matupu.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Mizari ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka Waarabu wanaosema المئزر al-mizar inayomaanisha "kimori, aproni" [3]

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Mizar" [4].

Dzeta Ursae Majoris ni jina la Bayer; Dzeta ni herufi ya saba katika alfabeti ya Kigiriki lakini Mizari ni nyota angavu ya nne na hii ni mfano ya kwamba Bayer hakufuata mwangaza kamili wakati wa kuorodhesha nyota.


Tabia[hariri | hariri chanzo]

Mizari ipo kwa umbali wa miaka nuru takriban 86 kutoka Jua letu. Mwangaza unaoonekana ni mag 2.27. Mtu mwenye macho mema anatambua kando yake nyota dhaifu zaidi inayoitwa Alcor hivyo Mizar na Alcor ni jozi maarufu ya nyota. Haijulikani bado kama ni nyota Maradufu hali halisi zilizoungwa pamoja kwa gravity au la.

Lakini kwa darubini Mizar yenyewe ilitambuliwa kuwa nyota maradufu. Galileo Galilei aliweza kuona sehemu zake mbili alipokuwa mtu wa kwanza wa kutazama nyota kwa darubini. Sehemu hizi mbili zinaitwa Mizari A na Mizari B.

Kwa kutumia darubini bora zaidi ilitambuliwa katika karne ya 19 ya kwamba Mizar A ni nyota mbili pia. Leo hii inajulikana kuwa Mizar ni mfumo wa nyota nne zinazoshikamana na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Kwa jumla ni ni jozi mbili za nyota yaani Mizar A 1+2 na Mizar B 1+2.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. vipimo kufuatana na Lyubimkov, Leonid S.; et al. (February 2010)
  2. ling. Knappert 1993
  3. Allen (1899) anadai uk. 440 ya kwamba kiasili Waarabu walitumia jina "Mirak" (mgongo), lakini jina lilibadilishwa katika tafsiri moja kwa Kilatini kuwa Mizar na jina hili liliendelea hata kutumiwa na Waarabu wenyewe baadaye. Kinyume ni Davis (1944PA) anayeandika jina ilikuwa kiasili "al-anaq" yaani mbuzi wa kike
  4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Christian A. Hummel et al.: Navy Prototype Optical Interferometer Observations of the Double Stars Mizar A and Matar. In: The Astronomical Journal. Bd. 116, Ausg. 5, 1998, S. 2.536–2.548.. online hapa
  • Davis, George R., Jr..: The Pronunciation, Derivations and Meanings of a Selected List of Star Names, Popular Astronomy, Vol. 52, p.8 00/1944 online hapa